Meneja mauzo na masoko wa Kampuni ya vinywaji baridi ya Nyanza Bottling Co. ltd Samuel Makenge akimkabidhi zawadi ya TV Bi. Mariam Simon mkazi wa Kisesa mtaa wa Mashariki A, baada ya kushinda kupitia shindano la Mchongo Chini ya kizibo.
Naye
Timo Juma Agustino mkazi
wa Misungwi mtaa wa Centre, anasema zari lake lilitokea kwenye sherehe ya mdogo wake aitwaye Charles wiki moja iliyopita ambapo baada ya kufungua soda na kupindua kizibo alikuta mchongo wa injini, ndipo kasi yake ya kusaka tairi la mbele na la nyuma ilipoanza, na hatimaye leo anaitwa mshindi.
Meneja mauzo na masoko wa Kampuni ya vinywaji baridi ya Nyanza Bottling Co. ltd
Samuel Makenge (kushoto) akimkabidhi zawadi ya TV Emmanuel Zacharia mkazi wa Buhongwa mtaa wa Mitimirefu, baada ya kushinda kupitia shindano la Mchongo
Chini ya kizibo.
Meneja mauzo na masoko wa Kampuni ya vinywaji baridi ya Nyanza Bottling Co. ltd
Samuel Makenge (kushoto) akimkabidhi zawadi ya pikipiki Lucas Gwanjingi mkazi wa Kisesa
mtaa wa Kitumba, baada ya kushinda kupitia shindano la Mchongo
Chini ya kizibo.
Meneja mauzo na masoko wa Kampuni ya vinywaji baridi ya Nyanza Bottling Co. ltd
Samuel Makenge (kushoto) akimkabidhi zawadi ya pikipiki Armes Issa mkazi wa Mkuyuni mtaa wa Shede, baada ya kuibuka mshindi kupitia shindano la Mchongo
Chini ya kizibo.
Meneja mauzo na masoko wa Kampuni ya vinywaji baridi ya Nyanza Bottling Co. ltd
Samuel Makenge (kushoto) akimkabidhi zawadi ya pikipiki Timo Juma Agustino mkazi
wa Misungwi mtaa wa Centre, baada ya kuibuka mshindi kupitia shindano la
Mchongo
Chini ya kizibo.
Meneja mauzo na masoko wa Kampuni ya vinywaji baridi ya Nyanza Bottling Co. ltd
Samuel Makenge (kushoto) akimkabidhi zawadi ya Tshirt, Enock Metusela mkazi
wa Igoma mtaa wa Kishiri, baada ya kuchungulia chini ya kizibo na hatimaye kujipatia zawadi yake, ni kupitia shindano la
Mchongo
Chini ya kizibo linaloendeshwa na kampuni hiyo..
Promosheni ya ‘Mchongo chini ya kizibo’iliyozinduliwa na Coca-Cola
mkoani Mwanza wiki iliyopita imekuja na kasi ya kipekee kwa kuibua washindi ambapo wakazi
wawili wa jijini Mwanza wamejishindia Televisheni na wengine wa 3
kujishindia pikipiki kila mmoja wao.
Promosheni hii inahusisha vinywaji vya Coca-Cola, Fanta, Sprite, Tangawizi,
Sparleta na Novida na inafanyika mkoani Mwanza na mikoa mingine ya kanda
ya ziwa ikiwemo mikoa jirani yake ya Shinyanga na Kigoma na
ikiwawezesha wateja kujishindia zawadi nono za fedha taslimu zaidi ya
milioni 400, bodabado 100, televisheni 60 aina ya SONY LED zenye inchi
32, T-shirts , kofia na soda za bure.
Akiongea
katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi jijini Mwanza, Meneja mauzo na masoko wa Kampuni ya vinywaji baridi ya Nyanza Bottling Co. ltd Samuel Makenge, alisema kuwa, imekuwa ni faraja kuona akinamama nao wanachomoza katika safu za washindi hali ambayo inadhihirisha kuwa mchezo huo upo kwaajili ya wanywaji wote.
"Napenda kusema kuwa hizi zawadi ni kweli, leo hii tunashuhudia tukiwapa wateja wetu zawadi ambazo ni pikipiki 3 na TV 2 ambapo hapo awali tulishatoa zawadi kwa washindi wengine, nazo zawadi za fedha taslimu za shilingi 100,000/= kwa kila mshindi ni kiasi cha shilingi takeibani milioni 2 zimeshatoka kwa wateja wanaofuata zawadi zao kiwandani.
“Rai yangu kwa wateja, usiache kizibo kikakupita, kila unapokunywa soda hakikisha unazibua kizibo usitupe kizibo"
Kuhusu swali lililoulizwa na moja wa waandishi kwamba kampuni inajisikiaje mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi Meneja huyo wa mauzo na masoko alisema "Nifaraja sana unapokuta kijana kama huyu anakiri kuwa hana ajira nasi tunampa kitendea kazi cha kumpatia ujira ni hali ambayo tunaona wazi kuwa nasi tunashiriki kubadilisha maisha yake"
Mmoja
wa washindi wa Lucas Gwanjingi mkazi wa Kisesa
mtaa wa Kitumba akiongea
kwa furaha alisema kuwa haamini macho yake baada ya kufika kiwandani hapo na kuzawadiwa pikipiki kwa kunywa soda 3 tu aina ya Coca-Cola zenye thamani ya shilingi 1,500/= na hatimaye kujinyakulia zawadi hiyo.
Makenge, amesisitiza
kuwa ili mteja kujishindia zawadi anatakiwa kubandua kiambatanisho
laini kilichopo chini ya kizibo cha soda.
Kwa upande wa fedha taslimu
kuna zawadi za shilingi 5,000/-, 10,000/- na 100,000 “Kwa upande wa
zawadi ya bodaboda anachotakiwa kufanya mteja ni kukusanya vizibo vitatu
vyenye picha zinazokamilisha picha ya bodaboda – kuonyesha upande wa
Nyuma, Katikati na Mbele na zawadi nyinginezo za Televisheni, kofia,
T-shirt na soda za bure zinapatikana chini ya kiambatanisho laini chini
ya kizibo kama zilivyo zawadi kubwa’’.
Amesema
zawadi zote kubwa zitatolewa kwa washindi kiwandani na zawadi
ndogondogo zitatolewa kwa mawakala wanaouza bidhaa za kampuni na magari
ya usambazaji vinywaji vya Coca-Cola.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.