Watetezi wa haki za binadamu kwa umoja wao wametaka watu wasiojulikana waweze kuchukuliwa hatua za kiusalama mara moja ili kubaini wahalifu hao wanajihusisha na vitendo vya kikatili dhidi ya watu mbalimbali nakuzuia hali hiyo isiendelee kutokea tena.
Akizungumza leo Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Sheria na Haki za binadamu, Dkt Helen Kijo-Bisimba amesema kwamba matukio hayo kukomeshwa kutajenga amani na umoja kwa watu.
Kama hatua za kisheria na za kiusalama hazitachukuliwa kwa tukio hili la kinyama litaleta shida kwa taswira ya nchi ya Tanzania kwenye nchi zingine na kuchafua serikali. Kwani hakuna nchi duniani iliyoingia katika kadhia hizi ni zikabaki salama" Bi Kijo-Bisimba
Pamoja na hayo watetezi hao wamemuunga mkono Rais kutokubali kunyonga baadhi ya wafungwa ambao wamehukumiwa kifo
Mbali na hayo Kituo hicho kimewataka viongozi wa dini kuchukua hatua madhubuti kukemea kwa nguvu kubwa matukio hayo kwani mwisho wa matukio haya ni kuvunjika kwa amani ya nchi. Pia amewataka viongozi wa siasa kujadili masuala ya usalama na haswa suala la utekwaji na mashambulizi ya kinyama kwa wananchi na kutoa mapendekezo yatakayoleta suluhu ya kudumu kwa usalama wa nchi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.