ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 10, 2017

MGOMBEA URAIS AKIRI KUSHINDWA KENYA, MMOJA AUAWA KITUO CHA UCHAGUZI KISII.

Mgombea urais wa kujitegemea katika uchaguzi mkuu wa Kenya amekiri kushindwa baada ya matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais kuonesha kuwa, ameshika nafasi ya sita kwa kupata kura elfu 11 na 256.

Bwana Japheth Kavinga amekiri kuwa, haoni kwamba ana nafasi ya kupunguza tofauti kubwa iliyopo baina yake na wagombea wengine wanaoongoza katika matokeo ya awali ya kura za uchaguzi wa rais uliofanyika jana kote nchini Kenya.
Matokeo ya awali yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi ya Kenya (IEBC) yanaonesha kuwa, mgombea wa chama cha Jubilee, Uhuru Kenyatta anaongoza kwa kura milioni saba na laki 9 na 63 elfu ambazo ni sawa na asilimia 53.89 ya kura zilizohesabiwa huku mpinzani wake mkuu, Raila Odinga akiwa na kura milioni sita na laki tano na sabini elfu ambazo ni sawa na asilimia 44.47 ya kura.
Wakati huo huo imeripotiwa kuwa polisi katika kaunti ya Kisii wamemuua kwa kumpiga risasi mtu mmoja nje ya Shule ya Sekondari ya Nduru ambayo ina kituo cha kuhesabu kura za uchaguzi wa rais katika jimbo la uchaguzi la Mugirango.
Wananchi wakiangalia maiti ya mtu aliyeuawa Kisii.
Watu walioshuhudia wanasema kuwa, mtu huyo alipigwa risasi mgongoni mapema leo na kwamba polisi aliyempiga risasi alihamishwa haraka kutoka eneo hilo.
 
Kamanda wa Polisi ya Kaunti ya Kisii, Abdi Hassan amesema polisi huyo ametiwa nguvuni.  

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.