WAKAZI
WA KITONGIJI CHA BUKALA KATA YA IBISABAGENI WILAYANI SENGEREMA WAMEIOMBA
SERIKALI KUWATATULIA KERO YA MAJI KATIKA
KATA HIYO INAYOENDELEA WAKATI MRADI MKUBWA WA MAJI UMESHAZINDULIWA WILAYANI
HUMO
Malalamiko hayo yametolewa na wakazi hao katika mkutano wa vitongoji vitano kwenye kata hiyo vilivyokaa kujadili jinsi ya kutatua kero mbalimbali katika eneo hilo likiwemo swala
la maji na kuiomba serikali kutatua changamoto hiyo
Wakizungumzia adha wanayoipata kutokana na kero hiyo bi
Pendo Doto na bi Mary Karoli wao wamesema inawalazimu kuamka saa tisa usiku kwenda kisimani, na kutanguliza ndoo zao na madumu hali ni mazingira hatarishi na siyo kuvamiwa tu bali pia baadhi yao wamewahi kuumwa na nyoka hali ambayo inawafanya kuishi maisha ya hofu.
Kwa upande wake balozi Faida Yusuph amesema mwenyekiti wa serikali ya mtaa amekuwa akiwalaghai kwa kuahidi kutatua kero hiyo na hadi sasa hakuna kilichofanyika
Nayebalozi Joseph
Agustine amekiri kuwepo kwa kero hiyo na kuongeza kuwa kumekupo gari la
serikali linalopitisha maji na kuyapeleka kwa watumishi waserikali wanaoishi maeneo hayo na kuwaacha wananchi wakiangaika
Aidha bwana Joseph amesema maji hayo ya kisima yanayotumika kwa sasa si safi na si salama na wananchi wako tayari kuchangia upatikanaji wa miundombinu ili kutatua kero hiyo
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.