ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 9, 2017

UHURU KENYATA AELEKEA KUIBUKA MSHINDI; UPINZANI WAKATAA MATOKEO.


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya anaelekea kupata ushindi katika uchaguzi wa Rais uliofanyika jana, huku muungano wa upinzani wa NASA ukiendelea kusisitiza kuyakataa matokeo hayo.
kwa mujibu wa matokeo rasmi ya kura zilizohesabiwa hadi tunaingia mitamboni, rais Kenyatta alikuwa anaongoza kwa kura milioni saba na laki saba ambazo ni sawa na asilimia 54  huku mpinzani wake mkuu Raila Odinga akiwa na kura milioni sita na laki tatu ambazo ni sawa na asilimia 44.7 ya kura. Matokeo hayo ni baada ya kuhesabiwa karibu asilimia 93 ya kura zote.

Mgombea urais wa muungano wa upinzani nchini Kenya National Super Alliance (Nasa) Raila Odinga amepinga matokeo ambayo yanaendelea kutangazwa na tume ya uchaguzi nchini humo, IEBC.

Bw Odinga amewaambia wanahabari kwamba tume hiyo imekuwa ikitangaza matokeo kwenye tovuti yake bila kufuata utaratibu ufaao.
Raila Odinga.
Akizungumza hivi punde na waandishi wa habari mjini Nairobi, Bwana Odinga amesema kuwa, upinzani una ushahidi unaoonyesha kwamba, chama tawala cha Jubilee kimeiba kura baada ya kuvurufa mitambo ya computa ya kutuma matokeo.

Awali wakala mkuu wa muungano huo wa upinzani, Musalia Mudavadi alihutubia wanahabari na kutaja matokeo yanayotangazwa na tume hiyo katika tovuti yake kama utapeli, huku akitoa wito kwa wafuasi wa mrengo huo kupuuzilia mbali matokeo hayo.

Ili kuibuka mshindi na kuepusha kuingia duru ya pili ya uchaguzi, mshindi wa uchaguzi wa urais nchini humo anahitaji kupata asilimia 50+1 ya kura, na kwa akali asilimia 25 kutoka kaunti 24, kati ya kaunti 47 za nchi hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.