Chama cha upinzani nchini Afrika Kusini cha
Democratic Alliance (DA) kimetoa wito wa kuvunjwa Bunge la nchi hiyo na
kufanyika uchaguzi mpya.
Wito
huo umetolewa siku moja baada ya kushindwa kwa hoja ya kambi ya
upinzani ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma wa nchi
hiyo.
Mkuu
wa chama cha upinzani cha DA, Mmusi Maimane amesema kuwa chama hicho
leo kitawasilisha bungeni hoja ya kulivunja Bunge na ameomba hoja hiyo
ijadiliwe haraka iwezekanavyo.
Rais
Jacob Zuma wqa Afrika Kusini ambaye anakabiliwa na tuhuma za ufisadi na
kutumia vibaya madaraka amenusurika kura ya kutokuwa na imani naye na
kuondolewa madarakani. Hata hivyo kiongozi huyo amejeruhika
kisiasa baada ya baadhi ya wanachama wa chama chake tawala cha ANC
kuungana na upinzani na kupiga kura dhidi yake.
Rais Zuma wa Afrika kusini ambaye amenusurika kura ya kuondolewa madarakani.
Rais Zuma wa Afrika kusini ambaye amenusurika kura ya kuondolewa madarakani.
Maimane amewaambia waandishi wa habari katika mji wa Cape Town kwamba
matokeo ya kura za wabunge yameonyesha kuwa, chama cha ANC
kimegawanyika na nchi inahitaji mwanzo mpya.
Mkuu
huyo wa chama cha upinzani cha Democratic Alliance amesema anaamini
kuwa, Bunge linapasa kuvunjwa ili nchi hiyo iitishe uchaguzi wa mapema.
Kipindi cha utawala wa Zuma kitamalizika mwaka 2019.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.