Mratibu
wa Uanzishwaji wa Mfuko wa Ubunifu Vijijini, Bw. Albert Ngusaru
akizungumza kabla ya ufunguzi wa mkutano wa siku moja wa kujadili namna
bora ya kuendeleza
Mfuko huo.
Mwakilishi
wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Adam Kamanda (kushoto)
akifungua mkutano wa siku moja wa kujadili namna bora ya kuendeleza
Mfuko wa Ubunifu
Vijijini huo.
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Adam Kamanda akieleza lengo la uanzishwaji wa Mfuko wa Ubunifu Vijijini.
Mshauri wa Kiufundi wa MIVARF, Bw. Ravi Malik akiwasilisha dhana ya uanzishwaji wa Mfuko wa Ubunifu Vijijini.
Mwakilishi
wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Adam Kamanda (kushoto)
akizungumza na Mratibu wa Uanzishwaji wa Mfuko wa Ubunifu Vijijini, Bw.
Albert
Ngusaru (kulia).
Mwezeshaji
wa Majadiliano ya Uanzishwaji wa Mfuko wa Ubunifu Vijijini, Bw. Severin
Ndaskoi (kushoto) akihimiza jambo wakati wa majadiliano hayo. Kulia ni
Meneja
wa Hazina na Ukwasi wa TADB, Bibi Beatrice Mrema.
Washiriki wa Mkutano wa Majadiliano ya Uanzishwaji wa Mfuko wa Ubunifu Vijijini wakifuatilia kwa umakini mkutano huo.
Washiriki wa Mkutano wa Majadiliano ya Uanzishwaji wa Mfuko wa Ubunifu Vijijini wakifuatilia kwa umakini mkutano huo.
Washiriki wa Mkutano wa Majadiliano ya Uanzishwaji wa Mfuko wa Ubunifu Vijijini wakifuatilia kwa umakini mkutano huo.
Washiriki wa Mkutano wa Majadiliano ya Uanzishwaji wa Mfuko wa Ubunifu Vijijini wakifuatilia kwa umakini mkutano huo.
WADAU WAKUTANA KUJADILI MFUKO WA KUENDELEZA UBUNIFU VIJIJINI
Na Mwandishi wetu,
Wadau
kutoka sekta za kilimo na uchumi wamekutana kujadiliana namna bora ya
uanzishwaji wa Mfuko wa Ubunifu Vijijini (rural innovation fund) wenye
lengo la
kuchochea, kuhamasisha na kusaidia uvumbuvi katika maeneo ya maendeleo
vijijini, ukopeshaji wa shughuli za kilimo na huduma za taasisi ndogo za
kifedha.
Mkutano
huo wa siku moja umeandaliwa kwa ushirikiano wa Benki ya Maendeleo ya
Kilimo Tanzania (TADB) na Programu ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji
Thamani
Mazao na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa TADB, Bw. Adam Kamanda amesema wadau wana mchango mkubwa wa
kutoa
maoni yatakayosaidia kuboresha usimamizi wa Mfuko huo ambao utakuwa
chini ya TADB.
“Nawaomba
tujadili namna bora itakayosaidia ndoto ya Serikali ya kuchagiza
upatikanaji wa fedha za gharama nafuu kwa ajili ya kuwasaidia wakulima
hasa katika
maeneo ya maendeleo vijijini, ukopeshaji wa shughuli za kilimo na
huduma za taasisi ndogo za kifedha,” alisema.
Bw.
Kamanda ameongeza kuwa uanzishwaji wa mfuko huu unalenga kutekeleza kwa
vitendo dhamira ya Serikali ya kutatua changamoto zinazoikabili sekta
ya kilimo
ambayo ni shughuli kuu kwa Watanzania wengi wanaoishi maeneo ya
vijijini.
“Uanzishwaji
wa Mfuko huu utasaidia bado ukuaji wa sekta ya maendeleo vijijini
ambayo imekuwa ukikabiliwa na changamoto mbali mbali kama vile kiwango
kidogo
cha uzalishaji; ukosefu wa mbinu na teknolojia za
kisasa; matumizi madogo ya umwagiliaji; ukosefu wa mtaji na upatikanaji wa mikopo kwa wakulima,” aliongeza.
Kwa
upande wake Mshauri wa Kiufundi wa MIVARF, Bw. Ravi Malik alisema
kuanza kazi kwa Mfuko huu kutasaidia changamoto za ukosefu wa masoko ya
mazao, miundo
mbinu mibovu ya usafirishaji, nishati ya umeme na miundombinu hafifu
vijijini hali itakayochochea ongezeko la thamani kwa mazao ya kilimo
maeneo ya vijijini.
Bw.
Malik aliongeza kuwa Mfuko huo utawezeshwa kwa kupatiwa mtaji wa Fedha
za Kimarekani (USD) zipatazo Milioni 5 ambazo zitatolewa kwa ushirikiano
wa Serikali
ya Tanzania kwa ushirikiano na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya
Kilimo (IFAD).
“Fedha
hizi zimelenga kukuza ongezeko la upatikanaji wa huduma za kifedha kwa
wananchi waishio vijijini kupitia njia mbalimbali za utoaji wa fedha
ikiwa ni
pamoja na huduma za mitandao ya simu ambazo zimekuwa kiungo muhimu
katika kuongeza ushirikishwaji wa kifedha kwa watu wasiotumia huduma za
kibenki,” aliongeza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.