Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (mbele katikati) akiongoza mkutano na wawakilishi wa Kampuni za Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba (wa pili kutoka kulia) akizungumza wakati wa mkutano. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Baadhi ya wawakilishi wa Kampuni za Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Nchini kwenye mkutano na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).
Mwakilishi kutoka Kampuni ya Ophir Energy, Halfan Halfan (katikati) akielezea maendeleo ya shughuli zinazofanywa na kampuni yake wakati wa mkutano wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na Kampuni za Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Nchini.
Baadhi ya wawakilishi
wa Kampuni za Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Nchini kwenye
mkutano na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo
pichani).
WAZIRI wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema mikutano ya kila baada ya miezi mitatu
na Kampuni zinazojihusisha na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia
Nchini itakuwa ikifanyika katika maeneo mbalimbali nchini hususan kwenye
rasilimali husika.
Waziri Muhongo
aliyasema hayo hivi karibuni Mkoani Mtwara wakati wa mkutano wake na
wawakilishi wa kampuni hizo uliofanyikia kwenye Kituo cha Kuchakata Gesi Asilia
cha Madimba.
Alisema mikutano husika
ilikua ikifanyikia jijini Dar es Salaam lakini ili kuleta tija zaidi,
imeamuliwa iwe inafanyikia kwenye maeneo yenye gesi asilia na baadaye siku za
usoni itafanyika kwenye maeneo yatakayogundulika kuwa na mafuta.
Aliongeza kuwa kila
baada ya miezi mitatu kumekuwepo na utaratibu wa kukutana kwa ajili ya kutathmini
tmaendeleo ya miradi husika na kila kampuni inawasilisha ratiba yake ya kazi
ambayo inajadiliwa.
“Hii mikutano kila
kampuni inatupatia ratiba yake ya kazi, tunaijadili na tunashauriana na kama
wana matatizo tunatafuta suluhisho,” alisema Waziri Muhongo.
Waziri Muhongo
alisema shughuli za Utafutaji, Uvunaji na Uendelezaji wa Gesi Asilia na Mafuta
zinaendelea vizuri huku majadiliano mbalimbali yakiendelea kuhusiana na
utekelezaji wa miradi husika.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.