ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 13, 2017

WATU 8 WAUAWA, KATIKA MLIPUKO WA BOMU MOGADISHU, SOMALIA


POLISI ya Mogadishu, mji mkuu wa Somalia imetangaza habari ya kuuawa watu wanane katika mripuko wa bomu uliotokea leo mjini humo.
Mripuko huo uliotokea karibu na hoteli moja katika mtaa wenye watu wengi mjini Mogadishu, umepelekea kwa akali watu wanane kuuawa na wengine saba kujeruhiwa na kuna uwezekano wa idadi ya wahanga ikaongezeka zaidi.
Athari ya hujuma za kigaidi nchini Somalia.
Hadi sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na mripuko huo, ingawa kidole cha lawama kimeelekezwa kwa wanachama wa kundi la kigaidi na kiwahabi la ash-Shabab ambalo limekuwa likitekeleza hujuma hizo.

Jumapili ya jana kulitokea mripuko mwingine mjini Mogadishu na kusababisha uharibifu wa mali na nafsi.

Kwa miaka kadhaa sasa, Somalia imekuwa uwanja wa mashambulizi ya kundi la kigaidi la ash-Shabab, lenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaidah. Wanachama wa kundi hilo ambao wanapigana na serikali ya Somalia, wanadai kuwa wanataka kuwaondoa nchini humo askari wa kigeni kutoka Kenya, Uganda, Ethiopia na Djibouti chini ya mwamvuli wa Umoja wa Afrika AMISOM.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.