Katibu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema leo katika mazungumzo na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam kwamba msafara huo utakuwa na wachezaji 20 pamoja na viongozi kadhaa ambao watatajwa baadaye.
Yanga imeanza mazoezi leo asubuhi kujiandaa na mchezo wa marudiano, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na mabingwa hao wa Zambia katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo wa juzi, uliochezeshwa na maarefa kutoka Djibouti, Djamal Aden Abdi aliyeyesaidiwa na Hassan Yacin na Farhan Salime, Yanga walitangulia kwa bao winga wake machachari, Simon Happygod Msuva dakika ya 39, kabla ya Zanaco kusawazisha dakika ya 78 kupitia kwa mshambuliaji wake Mghana, Attram Kwame.
Yanga sasa watalazimika kwenda kushinda ugenini katika mchezo wa marudiano mwishoni mwa wiki ili kusonga mbele hatua ya makundi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.