WATU wasiopungua 48 wakiwemo watoto 15
wamefariki dunia katika maporomoko ya udongo yaliyotokea kwenye dampo
kubwa la takataka nje kidogo ya mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. Hayo
yameelezwa na msemaji wa Halmashauri ya mji wa Addis Ababa.
Itafahamika kuwa
mamia ya watu wamekuwa wakiishi katika eneo hilo la jalala la Reppi
lenye umri wa miaka 50 wakisaka chakula na vitu vingine wanavyoweza
kuviuza kama vile mabaki ya vyuma n.k.
Amare Mekonen msemaji wa
Halmashauri ya mji mkuu, Addis Ababa amesema juhudi za uokoaji
zinaendelea ili kuwasaka watu ambao bado hawajulikani walipo tangu
kutokea maporomoko hayo ya udongo hapo juzi.
Watu wengine 20 wamapatiwa matibabu hospitali. Mekonen amesema kuwa,
watu ambao walikuwa wakiishi katika eneo hilo la dampo la taka hivi sasa
wamehamishiwa katika vituo vya vijana katika maeneo mengine ya Addis
Ababa.
Juhudi za uokoaji zikiendelea katika dampo hilo la taka lililoporomoka Addis Ababa |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.