HABARI kutoka nchini Marekani zinasema kuwa
kumezuka mapigano baina ya wafuasi na wapinzani wa Donald Trump katika
mji wa Berkeley wa jimbo la California, magharibi mwa nchi hiyo.
Televisheni ya Russia Today
imeripoti habari hiyo na kusema kuwa, mapigano hayo makali yamezuka
kwenye maandamano ya wafuasi na wapinzani wa Donald Trump huku baadhi ya
waandamanaji wakitumia mabomu ya moto dhidi ya wapinzani wao.
Watu kadhaa wamejeruhiwa kwenye mapigano
hayo ambapo kwa mujibu wa watu walioshuhudia, polisi hawakuchukua hatua
yoyote kuyazuia.
Maandamano dhidi ya Donald Trump nchini Marekani. |
California ni jimbo ambalo viongozi wake
wamekuwa wakifanya juhudi za kuwa huru katika siasa zao kuhusu
wahamiaji na kutofautiana na siasa za serikali kuu inayoongozwa na
Donald Trump.
Wapinzani wa siasa za Donald Trump
wanamtuhumu rais huyo wa Marekani kuwa ni mbaguzi wa rangi mwenye chuki
na watu wasio Wazungu.
Idadi ya wapinzani wa siasa hizo za
Donald Trump wanaongezeka siku hadi siku ndani na nje ya Marekani na
wanasema kuwa, tangu aingie madarakani huko Marekani, Trump amepelekea
kuzuka machafuko na hali ya wasiwasi mkubwa ndani ya jamii ya Marekani
na duniani kiujumla.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.