RAIS Magufuli leo mkoani Mtwara wakati akiweka jiwe la msingi katika
kituo cha kupooza umeme njia ya KV 132 amelipongeza Shirika la Umeme
nchini Tanesco na kumpongeza Waziri wa Nishati na Madini, kwa juhudi
zake katika kazi.
Rais Magufuli amesema aliamua kumteua Sospeter Muhongo kuwa Waziri
kutokana na ukweli kwamba alikuwa anaona uchapaji wake wa kazi kipindi
ambacho yeye ni Waziri wa Ujenzi.
"Lengo lililokuwa kwenye ilani ya Uchaguzi kwa mwaka jana ilikuwa
asilimia thelathini na kitu nyinyi mkafika mpaka asilimia arobaini, na
sasa hivi mko zaidi ya asilimia 46 sasa nisipowapongeza nitakuwa mtu
mbaya wa moyo mbaya.
"Na mimi na moyo mzuri kweli ndiyo maana nawapongeza wizara pamoja na
Tanesco haya matatizo mengine ambayo yanatokea ni kwa sababu tuliingia
mikataba ya hovyo huko nyuma, ya kulipia capacity charges ninajua
mnayashughulikia na tunajaribu kutafuta pesa za mikopo tulipe haya
madeni twende na Tanesco mpya" alisema Rais Magufuli
Mbali na hilo Rais Magufuli alimsihi Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo
"Nilipoteuliwa kuwa Rais sikuona mtu mwingine anayefaa kama Muhongo,
nikamrudisha hapa hapa sababu mimi nilipokuwa nikihesabu kilometa za
barabara yeye alikuwa anaesabu kilometa za nyaya, kwa hiyo nilifahamu
kazi yake na saa zingine ukifanya kazi vizuri unakuwa kama hupendwi
pendwi hivi, lakini kwa nini wakupende? Hata mke wako anaweza asikupende
siku zingine, wewe chapa kazi" alisisitiza Rais Magufuli
Rais Magufuli aliendelea kusisitiza kuwa katika maisha ya kila siku huwezi kupendwa na kila mtu
"Hata ndugu yako anaweza asikupende, saa zingine hata baba yako au
hata mdogo wako anaweza asikupende, huwezi ukapendwa na kila mmoja, hata
mitume hawakupendwa na wote na wengine walisulubiwa pamoja na kwamba
walifanya mazuri.
"Kwa hiyo Prof. Muhongo wewe fanyakazi tena usihangaike hata kusoma
ile mitandao, mimi sisomagi hiyo mitandao achana nayo watandae huko huko
wenyewe wewe chapa kazi" alisisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.