Nafsi yangu imenisukuma kushika kalamu na kuandika haya kutokana na kile kilichotokea Dodoma katika vikao vya CCM.
Ni takriban miezi 20 sasa toka nilipojitoa kutoka CCM, lakini nasikia bado naendelea kutajwa tajwa huko katika vikao vyao.
Wamewatimua wanachama na viongozi wao ambao wengi wao walitumia
demokasia yao kupinga upindishwaji wa kanuni na sheria za chama
chao.Nataka kuwaambia kuwa wakati wakifanya hivyo walikuwa mashujaa wa
haki na demokrasia na misingi ya utawala Bora nchini.
Hawa walikuwa mashujaa wa kutetea haki,demokrasia na taratibu na kupinga
dhulma ndani ya chama chao na nchini.Kwa kusimamia kile walichokiamini
bila ya kuvunja sheria, wamekata minyororo ya unyonge na uonevu.Mbegu
ile waliyoipanda itamea na kuzaa matunda demokrasia ya kweli nchini
kwetu.
Baba wa taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, kwamba upinzani wa kweli
utatokea CCM, naamini usemi huo sasa unatimia kwa kasi kubwa.
Nawakaribisha Chadema na UKAWA kwa jumla huku kuna maisha mazuri sana,
hakuna minyororo ya utumwa wa kisiasa. Kilichowapata ni sawa na kumpiga
chura teke unamuongezea kasi tu.
Waje wajiunge nasi katika safari ya kuleta Demokrasia ya kweli na siasa
zenye ukomavu,safari hii inahitaji umoja na mshikamano ili kufikia
malengo.
Huko wanajinasibu kuwa CCM ikiyumba, nchi itayumba lakini mimi nasema
kinachotokea ni kwamba, kwa jinsi CCM inavyoyumba, ndivyo wananchi
wanazidi kukomaa kisiasa na kuimarika katika harakati za kutafuta
mabadiliko ya kweli.
Watanzania wa sasa hawawezi tena kuvumilia ukandamizaji wa haki zao za
msingi unaofanywa na watawala. Nidhamu ya woga haina tena nafasi katika
kujenga nchi yenye kuheshimu misingi ya haki demokasia na utawala bora.
Edward Lowassa
Mjumbe kamati Kuu Chadema
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.