Baada ya kufunga magoli mawili kwenye mchezo wa Europa League wakati
Genk ilipocheza ugenini dhidi ya Gent, leo March 12, 2017 Samatta
ameendeleza moto wa kutupia kambani kwenye ligi kuu ya Ubelgiji kwa
kufunga goli moja wakati timu yake ikipata ushindi wa magoli 4-0 dhidi
ya KVC Westerlo.
Samatta alifungua nyavu za Westerlo mapema tu dakika ya 7 kipindi cha
kwanza, magoli mengine ya Genk yakafungwa na Thomas Buffel 27′, Omar
Colley 67’na Ruslan Manilovsky 90+2′.
Wafungaji wa magoli matatu ya leo, wote walifunga pia katika mechi ya
iliyopita ya Europa League (Samatta, Colley na Manilovsky).
Ushindi huo unaifanya Genk ifikishe jumla ya pointi 48 ikiwa katika
nafasi ya nane (8) kwenye msimamo wa ligi ya Ubelgiji inayoshirikisha
timu 16.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.