ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 16, 2017

MKURUGEZI WA MWAUWASA ASAINI MIKATABA YA ZAIDI BILIONI 240

ZEPHANIA MANDIA,MWANZA
 WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge amewataka Wakandarasi wa Miradi ya Maji  Safi na Usafi wa Mazingira kwa Jiji la Mwanza kuzingatia ubora katika kazi zao pamoja na kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa muda uliyopangwa.

Waziri Lwenge alisema hayo mkoani hapa wakati akisaini mikataba ya Ujenzi wa miradi hiyo, serikali kwa kushirikina na wadau wa maendeleo wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) pamoja na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).

“Miradi hii itajumuisha miji sita ambayo ni Mwanza, Musoma, Bukoba, Misungwi na Lamadi. Ninachotaka ni kwamba ikamilike kwa wakati na kazi ifanyike kwa viwango na ubora unaohitajika. Mtambue kuwa kiasi cha sh.bilionin 245 zitatumika kwenye  mradi huu,fedha hzio ni nyingi naomba kazi hiyo ifanyike kwa ufasaha,”alisema Mhandisi Lwenge.pia alimpongeza mkurugenzi wa mwuwasa injinia Anthon Sanga,kwakusimamia miradi mikubwa ya serikali.

Alisema Benki ya Maendeleo ya Ulaya pamoja na Shirika la Maendeleo la Ufaransa wanachangia sh. bilioni 105 kila mmoja ikiwa ni mkopo wenye masharti nafuu, ambapo Serikali ya Tanzania imechangia sh. bilioni 34 ambayo ni sawa na asilimia 14.

“Fedha hizi zinakusudiwa kunufaisha Jiji la Mwanza kwa kiasi cha sh.bilioni 133.7, Miji ya Bukoba na Musoma kwa kiasi cha sh.bilioni 62.5 na Miji ya Lamadi, Magu na Misungwi kiasi cha sh.bilioni 37.6, sh. bilioni 11.2 sawa na asilimia 5 zitakuwa ni gharama zitakazotumika katika usimamizi wa mradi,”alisema  Mhandisi Lwenge.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Mwanza (Mwauwasa), Antony Sanga.

Akizungumza baada ya kuwekeana saini hizo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Mwanza (Mwauwasa), Antony Sanga alisema: “Mradi huu utanufaisha idadi kubwa ya wakazi wa Mwanza. Tunaimani wale waliyokuwa wakikosa maji watapata vizuri. Maneo ya milimani nayo tunatarajiwa kuwa yatapata maji ya uhakika tofauti na ilivyokuwa awali.”
Lwenge alisema katika Jiji la Mwanza wakazi 105,649 wanaoishi katika maeneo ya miinuko watanufaika, wakazi wa Lamadi watakaonufaika ni 23,540, Magu 45,340 na Misungwi 23,315 na kwamba mradi huo utakamilika katika kipindi cha mizei 18.

“Kukamilika kwa miradi hii kutaongeza upatikanaji wa maji katika Jiji la Mwanza kutoka wastani wa asilimia 90 kwa eneo la mijini kwa sasa hadi kufikia asilimia 96 ifikapo 2019,”alisema.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.