ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 16, 2017

ELIMU IMEIPA MWANZA UJASIRI KUPIMA HIV BILA KUSUKUMWA.

Na James Timber,
GSENGO BLOG Mwanza
WATU
zaidi ya 400, mkoani Mwanza, wamejitokeza kupima virusi vya ukimwi sambamba njia ya uzazi wa mpango.

Hayo yalisemwa na  Mratibu wa Vijana wa Shirika la Marie Stopes Tanzania Daniel Mjema mara baada ya zoezi la  kuhudumia wananchi   la kupima afya kwa hiari, iliyotolewa na shirika hilo mtaa wa National kata ya Nyakato wilayani Ilemela mkoani hapa.

Mjema alisema kwa sasa muitikio wa watu ni  mkubwa ,kwani katika zoezi hilo lililofanyika kwa siku 3, watu  487 walijitokeza, huku wa uzazi wa mpango  261 na VVU 226.

Alisema, licha ya mwitikio kuwa mkubwa,watu wanatakiwa kujitokeza zaidi linapotokea suala la upimaji,ili waweze kupata huduma,elimu pamoja na kutambua afya zao.

Vijana wengi wamejitokeza katika zoezi la upimaji sambamba na makundi mbalimbali, kwani kupima na kutambua afya ni bora, kuliko kusubilia mpaka kuugua,hivyo jamii inatakiwa kuendelea kujitokeza endapo kunatokea huduma ya upimaji, " alisema Mjema.

Pia alisema, shirika hilo linawafikia  na watu vijijini kupitia huduma yao ya vikoba,licha ya kukutana na changamoto ya mila potofu.

Hata hivyo alisema, wanapita vyuoni, ili kuhamasisha vijana kupima afya zao, sambamba na kuelimisha juu ya afya ya uzazi na utumiaji njia ya uzazi wa mpango.

Aidha alisema, kuna sheria zinazo wabana, ili waweze kuanza kutoa elimu ya afya ya uzazi na VVU, kuanzia shule ya msingi, kwani wao ndio waathirika zaidi katika suala la mimba za utotoni.

Kadhalika alisema, shirika hilo na mashirika mengine,wanaendelea kuishawishi serikali, ili iwapatie kibali kwa ajili ya kutoa huduma hiyo kwa vijana wa shule za msingi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.