Halmashauri ya wilaya ya Sengererma imezindua vitambulisho kwa wazee ili kupata matibabu bure
Akizungumza na wazee hao katika kata ya IGALULA wilayani humo mkuu wa wilaya ya Sengerema mh Emanuel Kipole amewataka wananchi kufanya kazi ilikuleta maeendeleo ya taifa kwa kuwa serikali ya awamu ya tano inawataka watu wafanye kazi.
cue in MH KIPOLE 01 KAZI
Mh kipole amewapongeza wazee hao na kusema kuwa serikali inatambua mchango wa wazee na busara pia katika kulitumikia taifa na hata kupigania uhuru hivyo itaendelea kuwaenzi wazee hasa upande wa afya kwakuwa mtaji mkubwa wa maisha ya mwanadamu ni afya.e
Akizungumzia mpango wa serikali kwa wazee mh.Kipole amsema kuwa wazee wote kuanzia umri wa miaka 60 serikali itahakikisha wanapata huduma za afya bure bila malipo ,na zoezi hili la vitambulisho limeanza mwaka jana na tayari wazee 2001 wamekisha kupatiwa vitambulisho na bado linandelea.
Akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa wilaya ya Sengerema Magesa Mafuru Bonifasi amesemakuwa zoezi hili nimefanyika kwa ufanisi, na kufanikiwa kuwahamasisha wazee 651 na wazee 51 watakabidhiwa vitamburisho kwa kuwawakilisha wazee wengine katika kata nyingine na kuongeza kuwa katika zoezi hili mabalaza mbali mbali yameundwa kuanzia kijiji ,kata na mbalaza la wazee la wilaya.
Naye mganga mkuu wilaya Sengerema Dr .Petel Mangu amesema kuwa kazi hii ni kutekeleza maelekezo ya serikali kwa kuanzisha baraza na kutengeneza kumbukumbu za wazee katika wilaya na kuwapatia vitamburisho kwa huduma za matibabu na tayari wamefanikiwa kuunda baraza la wazee kwa ngazi ya kijiji na kata wakichuchumilia ngazi ya wilaya.
Idara ya afya Halmashauri ya Sengerema imepanga kutengeneza vitamburisho 651 kwa miezi 6, na kwamiezi zita ijayo vitatengenezwa vitamburisho 651 na vitamburisho vilivyotengenewa ni kwa kata 13 kati ya kata 26.
Nao wazee wametoa maoni yao kwa kuipongeza serikali kwa kuwaajali wazee changamoto ni upatikanji wa dawa katika hospitali
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.