ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 23, 2017

AFISA MWANDAMIZI WA MAREKANI ATIMULIWA KWA KUMKOSOA TRUMP.


Craig Deare, afisa mwandamizi katika serikali ya Marekani ametimuliwa kwa kukosoa sera za Rais Donald Trump wa nchi hiyo.

Deare, ambaye ni afisa mwandamizi wa Baraza la Usalama wa Taifa ameachishwa kazi baada ya kukosoa sera za Trump na washauri wake wa karibu.

Afisa huyo mwandamizi wa serikali ya Washington ambaye aliteuliwa mwezi uliopita kuongoza kitengo cha baraza hilo katika eneo la Hemisphere ya Magharibi alisindikizwa na maafisa wa usalama kutoka jengo la ofisi aliyokuwa akifanya kazi mjini Washington.

Afisa mmoja mwandamizi wa Ikulu ya White House amethibitisha kuwa Deare si mfanyakazi tena wa Baraza la Usalama wa Taifa na kwamba amerejea kwenye shughuli yake ya hapo kabla katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Ulinzi.

Afisa huyo amethibitisha ripoti hiyo kwa sharti la kutotajwa jina lake pasina kutoa maelezo zaidi.
Hata hivyo baadhi ya maafisa wa serikali ya sasa na ya zamani ya Marekani wamesema, Craig Deare amefukuzwa kufuatia matamshi aliyotoa siku ya Alkhamisi iliyopita katika kikao cha faragha kilichofanyika kwenye kituo cha tanuri fikra cha Wilson kilichoko mjini Washington.
Rais Donald Trump wa Marekani.
Kwa mujibu wa mmoja wa watu waliohudhuria kikao hicho, Deare aliishambulia vikao serikali ya Trump kutokana na sera zake kuhusiana na eneo la Amerika ya Latini  hususan kwa kuanzisha mikwaruzano na serikali ya Mexico.


Katika wiki ya kwanza mara baada ya kuingia madarakani, Rais wa Marekani alisaini dikrii ya ujenzi wa ukuta katika mpaka wa pamoja wa nchi hiyo na Mexico, ikiwa ni kutekeleza ahadi aliyotoa wakati wa kampeni za uchaguzi.

Hatua hiyo ilimfanya Rais Enrique Pena Nieto wa Mexico avunje safari yake ya kuelekea Marekani aliyokuwa amepanga kuifanya mwishoni mwa mwezi Januari.

Imeripotiwa kuwa Deare alionyesha waziwazi kukasirishwa na kukatwa mijadala yote ya sera kuhusiana na Mexico na kueleza kwamba washauri wa karibu wa Trump akiwemo mkuu wake wa stratijia Steve Bannon na mkwe wa Rais huyo Jared Kushner hawakuwasiliana na kurugenzi ya Baraza la Usalama wa Taifa wakati serikali ilipokuwa ikiandaa sera.../


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.