RAIS mpya wa Somalia, Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo ameapishwa leo mjini Mogadishu katika sherehe iliyohudhuriwa na viongozi wa nchi kadhaa za kanda hiyo chini ya hatua kali za ulinzi.
Baada ya kuapishwa Rais mpya wa Somalia ameahidi kurejesha heshima ya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika lakini pia ameonya kwamba, itachukua miongo miwili kurekebisha nchi hiyo.
Amesema Somalia inakabiliwa na changamoto nyingi na kwamba mafanikio ya serikali yake yatakuwa madogo kutokana na rasilimali zake chache.
Mohamed Farmajo amesema Somalia imekuwa katika vita kwa kipindi cha miaka 26 iliyopita ikisumbuliwa na migogoro na ukame na kwa msingi huo itachukua miaka 20 kurekebisha nchi hiyo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.