Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli ameweka wazi sababu ya kuteua mwanamke katika nafasi ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, kuwa ni kutokana na kwamba wanawake wengi ni waaminifu katika suala la fedha.
Kamishna Jenerali Dkt. Anna Peter Makakala , Jenerali wa Uhamiani Tanzania baada ya kiapo
Mhe. Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 12 Februari, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kumuapisha Dkt. Anna Peter Makakala kushika nafasi hiyo.
Wengine walioapishwa leo ni pamoja na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Rogers William Siyanga, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mhe. Joseph Edward Sokoine, Balozi wa Tanzania nchini Algeria Mhe. Omar Yusuf Mzee na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Grace Aaron Mgovano.
Mara baada ya kumuapisha, Rais Magufuli amemtaka Kamishna huyo kufanya mabadiliko makubwa ndani ya Idara ya Uhamiaji nchini kutokana na utendaji wake kutoridhisha.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.