RAIS Donald Trump wa Marekani ameanza kuchoshwa na uzito wa uendeshaji mambo katika Ikulu ya White House ikiwa ni wiki tatu tu tokea aapishwe.
Kwa mujibu wa jarida la Politico toleo la Ijumaa, bilonea Trump amepandwa na hasira baada ya kuona ukweli wa mambo katika mfumo wa serikali ya Marekani ambayo hawezi kuiendesha kama biashara zake.
Wapambe wa Trump wamenukuliwa na jarida hilo wakisema kuwa Trump amekumbwa na hali ngumu katika kazi za kusimamia biashara ya kifamilia hadi kuwa rais. Wapambe hao wa Trump ambao hawakutaka majina yao yatajwe wanasema Trump amekasirishwa na kuchoshwa na urasimu mkubwa katika serikali kuu ya Marekani hasa muda mrefu unaochukuliwa na bunge la Congress kuidhinisha mawaziri wake.
Ikulu ya White House. |
Aidha Trump amekerwa na kesi ambazo zimepelekwa mahakamani kupinga maamuzi yake tata hasa kuwapiga marufuku watu kutoka nchi saba za Kiislamu kuingia Marekani.
Aidha duru zinasema kuna wasiwasi miongoni mwa wafanyakazi wa White House ambao wengi hawajui majukumu yao huku kukikosekana motisha kazini, malumbano na uchovu.
Rais wa Marekani pia anakabiliana na maandamano ya Wamarekani na walimwengu kwa ujumla wanaopinga sera zake za kibaguzi.
AAAA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.