Wastaafu nje ya Ghand Hall. |
.
NA ANNASTAZIA MAGINGA, MWANZA.
BAADHI ya wastaafu wanaofanyiwa uhakiki hivi leo na Wizara ya fedha na mipango jijini mwanza wameiomba serikali kuboresha pesheni zao kutokana na gharama za maisha kupanda.
Wakizungumza na Gsengo blog kwa nyakati tofauti wamesema licha ya serikali kuamua kuwalipa mafao yao kila mwezi badala ya miezi mitatu lakini bado fedha hiyo haikidhi mahitaji na kwamba wanaomba waongezewe kiwango fulani cha fedha kwenye pesheni zao ili kusaidia kuendesha maisha.
Mmoja wa wastaafu hao Jumanne Bambe ameomba fedha hizo zifike kwa kwa wakati ili mtu aweze kutatua matatizo yake yanayomkabili kuliko kusubilia huku akiendelea kulimbikiza madeni yanatakayokuja kulipwa na pesheni.
“Uamuzi huu ni mzuri utatusaidia kutatua matatizo yetu kwa mwezi kuliko ya miezi mitatu pamoja na kulipwa pesheni zetu basi na sisi watujali angalau ile asilimia ya mishahara tusaidiwe kwani pia pesheni yangu iko kwenye uzalishaji sio kwamba imekaa tu kwa hiyo waliangalie na hili”amesema Bambe.
Aidha Wiazra ya fedha na mipango imezindua leo zoezi la uhakiki kwa wastaafu katika mikoa ya kanda ya ziwa ili kupata takwimu iliyo sahihi pamoja na kuwezesha serikali kulipa wastaafu wanaostahili.
Akizungumza na waandishi wa leo jijini Mwanza Mkaguzi mkuu wa ndani, msaidizi wa serikali Stanslaus Mpembe amesema lengo la uhakiki huo ni kuiwezesha wizara ya fedha na mipango kujua idadi ya wastaafu wanaolipwa ikiwemo viwango vyao na maeneo wanayopatikana.
Amesema wastaafu hao watahitajika kufika na nyaraka zitakazo mtambulisha na kwamba ambao hawataakikiwa wataondolewa kwenye orodha ya malipo ya pesheni.
“Wastaafu wanatakiwa kufika na Barua ya tuzo la kustaafu,Barua ya kustaafu au kupunguzwa kazini,Nakala ya hati ya malipo ya kiinua gongo au mkopo,Barua ya ajira ya kwanza,Kitambulisho cha pesheni,Barua ya kuthibitishwa kazini,Kadi ya Benki na picha ndogo mbili hivyo tunatoa wito waastafu wote kujitokeza kwa wingi ili kuhakikiwa”amesema Mpembe.
Zoezi hilo limeanza Oktoba 10 mwaka jana katika Mkoa wa Pwani ikifuatiwa na mikoa ya kanda ya kati,nyanda za juu kusini na kanda ya ziwa kuanzia leo Januari 9 ambapo litaendelea hadi januari 13 mwaka huu na kufuatiwa na mikoa ya Kigoma na Tabora januari 16 hadi 20 .
Maafisa wa ukaguzi wakipokea taarifa za wastaafu. |
Maelezo ya kina yakitolewa. |
Maafisa shughulini nao wastaafu mezani wakiwasilisha taarifa zao. |
Kwa mkoa wa Mwanza shughuli ya uhakiki inaendelea hapa Ghand Hall ambapo wastaafu wamejitokeza wa wingi kuhakikisha wanahakikiwa. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.