John Kerry, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani. |
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amekiri kuwa lengo lao kuu la kuanzisha genge la kigaidi la Daesh (ISIS) ni kuipindua serikali ya Rais Bashar al Assad wa Syria. Amesema, Washington iliruhusu kuanzishwa kundi la ISIS ili kufanikisha jambo hilo.
Vyombo mbalimbali vya habari vimemnukuu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani akiashiria kwamba nchi yake ilikuwa na matumaini kwamba kwa kuanzisha kundi la Daesh na kuliitia nguvu, itaweza kumpindua Bashar al Assad na baadaye kupata njia ya kidiplomasia yenye manufaa kwa Washington kuhusu suala la Syria na ni kwa sababu hiyo ndio maana Marekani iliwapa silaha baadhi ya wanamgambo wa ISIS.
Amesema, Washington ilikuwa inafuatilia sekunde kwa sekunde namna kundi la Daesh linavyopata nguvu na kuongeza kuwa, Marekani haikutarajia kuwa serikali ya Syria itaomba msaada wa kijeshi wa Russia.Marekani imeanzisha na kuyapa silaha magenge ya kigaidi ili kuzusha fitna katika safu za Waislamu. |
Mkanda wa sauti ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ambao ulirekodiwa wakati John Kerry alipokuwa anazungumza kwenye kikao na wajumbe wa makundi ya wapinzani wa Syria, umerushwa hewani na televisheni za CNN na kusambazwa pia na mtandao wa gazeti la New York Times.
Hata hivyo dakika 35 za mkanda huo ambazo zinazungumzia uungaji mkono wa Marekani kwa genge la kigaidi la Daesh zimechujwa na kutolewa na mashirika hayo ya habari ya Marekani.Ili kutilia nguvu matamshi ya rais mteule wa Marekani Donald Trump kuhusiana na kitendo cha Washington cha kuanzisha genge la kigaidi la ISIS wakati wa urais wa Barack Obama huko Marekani, mtandao wa WikiLeaks ulisambaza mitandaoni mkanda wa sauti ya John Kerry wakati alipoonana na wajumbe wa makundi ya wapinzani wa serikali ya Syria tarehe 22 Septemba mwaka jana.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.