VYA
HABARI LEO TAREHE 9.01.2016
·
WATU
WAWILI WAMEFARIKI DUNIA NA WENGINE WATATU KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA GARI
ILIYOHUSISHA ROLI LA MIZIGO NA GARI DOGO AINA YA SUBARU FORESTER SALOON
WILAYANI MAGU.
·
MTU
MMOJA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MISUNGWI.
KWAMBA MNAMO TAREHE
8.01.2017 MAJIRA YA SAA 06:10HRS ASUBUHI KATIKA KIJIJI CHA KISESA ENEO LA KONA
YA KAYEZE BARABARA YA MWANZA – MUSOMA WILAYANI MAGU MKOA WA MWANZA, WATU WAWILI
WALIOJULIKANA KWA MAJINA YA 1. DANIEL JOACKIM @ NYAMBO MIAKA 33, MFIPA NA 2. JANET
ADEN @ KAGOSA MIAKA 22, MJALUO, WAMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO NA WENGINE WATATU
KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA GARI ILIYOHUSIAHA LORI LA MIZIGO LENYE NAMBA T.575
BAT AINA YA SCANIA TRUCK LENYE TELA LENYE NAMBA 270 AKK LILILOGONGANA NA GARI
DOGO LENYE NAMBA T. 480 CAS AINA YA SUBARU FORESTA SALOON LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE DANIEL JOACKIM AMBAYE ALIFARIKI DUNIA KATIKA
AJALI HIYO.
MAJERUHI WA AJALI HIYO
NI 1. ADEN KAGORA MIAKA 55, MJALUO, 2. MICHAEL JOSEPHAT KAGOSA MIAKA 15 NA 3.
VICTORIA KAGOSA MJALUO MIAKA 13, WOTE NI ABAIRI WA GARI NDOGO LENYE NAMABA T.
480 AINA YA SUBARU FORESTA SALOON, AIDHA
HAKUNA DEREVA AU ABIRIA WA LORI ALIYE JERURIHIWA AU KUPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI HIYO.
CHANZO CHA AJALI NI
MWENDO KASI WA DEREVA WA GARI DOGO AMBAYE ALISHINDWA KULIMUDU GARI ALIPOKUWA
KWENYE KONA YA ENEO LA KAYEZE NA KUSABABISHA AJALI, MAJEERUHI WAMELAZWA
HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO NA HALI
ZAO ZINAENDELEA VIZURI, MIILI YA MAREHEMU PIA IMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO
PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ITAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA
MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA RAI KWA WAENDESHAJI WA
VYOMBO VYA MOTO AKIWATAKA KUWA MAKINI WAKIZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI PINDI WANAPOKUWA BARABARANI ILI KUEPUKA VIFO NA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA. AIDHA ALIWATAKA ABIRI KUTOA TAARIFA
MAPEMA POLISI PINDI WANAPOONA VIASHIRIA VYA MWENDO KASI ILI HATUA
ZICHUKULIWE HARAKA KABLA MADHARA HAYAJATOKEA.
KATIKA
TUKIO LA PILI
KWAMBA TAREHE
08.01.2017 MAJIRA YA 22.30HRS USIKU KATIKA BARABARA YA MWANZA – SHINYANGA ENEO
LA KIKIJI CHA USAGARA KATA NA TARAFA YA USAGARA WILAYA YA MISUNGWI MKOA WA
MWANZA, GARI NAMBA SU 40653 AINA YA
TOYOTA HILUX MALI YA SHIRIKA LA TENESCO MKOA WA MWANZA LILILOKUWA LIKIENDESHWA
NA DEREVA AITWAYE WEREMA IKWEBE MIAKA 35 MKAZI WA IGOGO TANESCO LIKITOKEA
MWANZA KWENDA SHINYANGA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU AMBAYE HAJAFAHAMIKA JINA
WALA MAKAZI ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI KATI YA MIAKA 50 HADI 55, WAKATI AKIVUKA
BARABARA NA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO.
CHANZO CHA AJALI NI
MWENDO KASI WA DEREVA GARI ALIYESHINDWA KULIMUDU GARI NA KUSABABISHA AJALI HADI
KIFO, DEREVA WA GARI HILO AMEKAMATWA PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA
MAHAKAMANI, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA CHA MISASI KWA AJILI
YA UCHUNGUZI NA UTAMBUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKALIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA
MAREHEMU KWA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAENDESHAJI WA
VYOMBO VYA MOTO AKIWATAKA KUZINGATIA ALAMA NA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI, LAKINI
PIA ANAWATAKA WATEMBEA KWA MIGUU KUWA MAKINI WAKATI WOTE PINDI WANAPOKUWA
BARABARANI ILI KUEPUSHA VIFO VINAVYOWEZA KUEPUKIKA.
IMETOLEWA NA,
DCP: AHMED
MSANGI
KAMANDA WA
POLISI (M) MWANZA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.