Wananchi wakerwa na Kamati kuhusu uchangiaji wa Elimu
Na James Timber, Mwanza
Baadhi ya wananchi wakerwa na Taarifa zilizotolewa na Viongozi wa Kamati katika Kikao cha Maendeleo ya Elimu katika Kata ya Bugogwa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Bugogwa Bw. Wiliam Mashamba aliiitisha kikao hicho wiki iliyopita katika viwanja vya shule ya msingi Bugogwa kilichokuwa na lengo la kuchangia suala la elimu katika kuongeza madawati kwa shule sita za msingi kata hiyo ambazo ni Kabangaja, Igombe, Isanzu, Kilabela, Bugogwa na Kisundi pamoja Shule ya Kata ya Sekondari ya Bugogwa.
Bw. Mashamba alieleza kuwa kila Kaya kati ya kaya 6000 ichangie shilingi elfu tano kwa ajili ya kuongeza madawati kwa shule sita za msingi na moja ya sekondari.
Hata hivyo wananchi walipinga kauli ya diwani huyo kwa kudai kuwa hakuna aliye tayari kuhusika na changizo hilo kwa sasa kwani ni njama ya viongozi kuzitafuna fedha za wananchi na kikao kuvurugika kwa mabishao makali kwa wananchi na mwenyekiti huyo bila muafaka kupatikana.
Diwani huyo alizidi kulaumiwa na wananchi hao wakimtaka aachane na suala la mchango kwanza mpaka atakapowaletea mapato na matumizi ya Miradi ya Shule hizo ili wawe na uhakika na mchango huo mpya unaowasilishwa, suala lililopigwa na baadhi ya wanakamati.
Aidha hapo awali Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ilichangia Kata hiyo madawati 536 na madawati 139 yakitoka kwa Mbunge wa jimbo la Ilemela Angelina Mabula.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.