ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 10, 2017

RONALDO MCHEZAJI BORA FIFA, RANIEL KOCHA BORA

Supastaa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ametangazwa kuwa mwanasoka bora wa FIFA na kuwabwaga Lionel Messi wa Barcelona na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid.
"Wow, wow, wow," Ronaldo alisema baada ya kunyakuwa tuzo yake.
"Ni ajabu" - siyo mara ya kwanza lakini kwangu hii ndiyo tafsiri ya tuzo yangu ya awali.
"Napenda kuwashukuru wachezaji wenzangu, kikosi kizima cha Real Madrid na shukurani kwa kila mlichofanya.
"Mwaka 2016 ulikuwa mwaka wangu wa mafanikio katika tasnia yangu. Nilikuwa na maswali mengi na mashaka, lakini tuzo zimedhihirisha jinsi nilivyokuwa nikiishi kwa matarajio yapi" 
Ronaldo na Messi kwa kipindi kirefu sasa wamekuwa kwenye mchuano wakipambanishwa yupi yu bora kuliko mwenzake, mwisho wa siku ni Ronaldo ndiye aliye likwea jukwaa lile na kuinyakuwa tuzo.

Kocha wa Leicester City Claudio Ranieri naye ameibuka kidedea kwa kuchaguliwa kuwa kocha bora wa FIFA. Kikosi cha wachezaji bora 11 wa FIFA nacho kimetajwa ambapo kwa mara nyingine wachezaji wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) wamesheheni katika orodha hiyo.

 Nyota wanaounda kikosi cha FIFA ni  Manuel Neuer, Dani Alves, Marcelo, Gerard Pique, Sergio Ramos, Andres Iniesta, Toni Kroos, Luka Modric, Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Luis Suarez. Ukiondoa kipa Manuel Neuer wa Bayern Munich na beki Dani Alves wa Juventus, wengine wote waliosalia wanatokea La Liga. 


Ligi yenye mashabiki wengi duniani - Premier League ya England, haijatoa hata mchezaji mmoja.


Mtoto wa Ronaldo - Cristiano Ronaldo Jnr akishika tuzo ya baba yake kwa shauku huku dada wa Ronaldo Elma akishuhudia

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.