ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, January 1, 2017

PROF JAY AUAGA MWAKA KWA KUMVISHA PETE GRACE.

Mbunge wa jimbo la Mikumi ambaye pia ni msanii wa muziki wa Bongo fleva Prof Jay ameitumia vyema siku ya kuuaga mwaka 2016 kwa kumvisha pete ya uchumba mzazi mwenzake Grace Mgonjo zikiwa ni harakati za kuelekea kufunga ndoa.
Prof Jay mwaka jana kupitia kipindi cha Planet bongo aliahidi na kusema kuwa haitapita muda mrefu sana watu wataanza kupewa kadi kwa ajili ya ndoa yake na sasa hizi ni dalili kuwa huenda ndoa hiyo ipo siku za karibuni.

"Asante sana Mungu, leo (Jana) tunaufunga mwaka namna hii na Mke wa Profjize" aliandika Prof Jay katika picha akiwa anamvisha pete ya uchumba Grace Mgonjo na picha ameiainisha kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Zaidi ya hapo Gsengo Blog inamtakia kila la kheri katika hili la kifamilia zaidi kwani furaha ya bwana ni kuwa na bibi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.