Zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya Serikali mkoani Mwanza, kuwahamisha katikati ya Jiji wafanyabiashara wadogo (Machinga), ifikapo Desemba 3 mwaka huu, akina mama wauza samaki na mama lishe mkoani humo wameangua vilio wakiomba kutohamishwa.
Wakina mama hao waliotanda mbele ya Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Nyamagana, wamelia wakiiomba Serikali kutowahamisha katikati ya Jiji, kutokana na madai kuwa miundombinu ya maeneo waliyotengewa kwa ajili ya kibiashara si rafiki.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment