ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 30, 2016

MATUKIO YA UPORAJI NA UJAMBAZI MWANZA: SASA NI MCHANA KWEUPEE TENA KATATIKATI YA ENEO LA MABENKI.

Mmoja kati ya wajeruhiwa huyu ni mfanyabiashara wa mashati ya mitumba ambaye hufanya biashara nje ya mgahawa wa Diners (Diners Restaurant) ulioko katikati ya jiji la Mwanza, ukitizamana na benki ya NMB Mwanza (upande wa pili wa barabara) hatua kama 20 za miguu, amejeruhiwa na risasi chini ya tumbo na haijaeleweka zaidi hali yake inaendeleaje hadi tulipokuwa tunaenda mtamboni.
Licha ya mgahawa huo kuwa katikati ya jiji la Mwanza lenye ulinzi madhubuti, mgahawa ukitizamana na benki ya NMB tawi la Kenyata yaani upande wa pili ukivuka barabara (hatua kama 20 za miguu) ni maeneo hayo hayo kuna Benki ya KCB na CRDB zenye vikosi vya ulinzi maeneo yake yote ya nje na ndani. 

Majambazi walifika katika mgahawa huo wakiwa kwenye pikipiki huku mmoja kati yao akiwa amevaa koti refu, walishuka na kuingia ndani ya mgahawa huo wakijifanya kutaka kupatiwa huduma ya chakula kama wateja wengine, humo ndani walimkuta mpishi Bwana Bagwani Dakante akiwa na ndugu yake aitwaye Surbir Kantula wamekaa wakiongea kwani kipindi hicho huduma ya chakula haikuwepo.

Ndipo jambazi mmoja aliyekuwa amevaa koti alichoma silaha na kuwatishia na kuwataka watoe pesa, waliwapa funguo na kuwaambia wakachukuwa wakachukue fedha kwenye sanduku pindi majambazi walipokuwa wanahangaikia funguo, ndipo Bagwani na mwenzake walipopata upenyo na kukimbia kupitia mlango wa nyuma.

Kutokana na hali hiyo majambazo hao walistuka kuwa wanaweza kukamatwa waliacha kuhangaika na funguo na kutaka mikakati ya kutoka eneo la tukio.

Walifyatua risasi tatu kuelekea mlango wa mbele na kuvunja kioo, risasi ambayo ilimpata Sltani Tugai ambaye alikuwa nje, vilevile nyingine ikampata Bagwani Dakante aliyekuwa tayari amefika mbele ya mgahawa akiwaelekeza watu kwamba ndani wapo wezi.

Majambazi hao walifanikiwa kutoka ndani ya mgahawa huo na kutimua eneo la tukio wakitumia pikipiki.

Tukio hili la ujambazi linakuwa ni tukio la tatu kutokea katika jiji la Mwanza ndani ya wiki mbili, Baadhi ya mashuhuda walikuwepo kwenye tukio ilo wamelaumu jeshi la polisi kwa kushindwa kufika katika eneo la tukio mapema licha ya kuwa tukio ilo lilitokea katikati ya maeneo ya ofisi zinazolindwa na jeshi la polisi ila pia ni mita takribani 100 kutoka kilipo kituo kikuu cha kati cha mjini Mwanza .










Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment