| Watangazaji kipindi cha Radio Jembe Fm Mwanza 'KAZI NA NGOMA' G. Sengo kulia akifunguka na kwa umakini mtangazaji mwenzake Mansour Kumanne akisikiliza kwa kina, hisiani akiandaa hoja. |
Viongozi wa makundi toka vituo mbalimbali Mwanza wamevamia studio za Jembe Fm Mwanza na kuwasilisha hoja zao na malalamiko yao ikiwa ni pamoja na vielelezo vya mikataba iliyofanyika siku za nyuma baina yao na halmashauri ya jiji la Mwanza.
Wafanyabiashara hao kwa pamoja wameridhia kutoondoka katika maeneo yao ya biashara mpaka mpango madhubuti na wakueleweka utakapoandaliwa na kuridhiwa na pande zote mbili.
"Na sisi tunasema hiyo siku ya tarehe 2 Desemba watatukuta bila mjadala. Machinga wote walioko kwenye maeneo yao, tutalala kwenye maeneo yetu kuanzia kesho alhamisi tarehe 1, na kinamama lishe watakuja na mtoto wao kulinda biashara zao........Hayo mabomu watapigwa mama na mtoto"
ZAIDI TIZAMA VIDEO HII HAPA
KUMBUKUMBU:- TAREHE 9 AGOSTI 2016 HAYA YALIZUNGUMZWA NA MHE. RAIS
RAIS MAGUFULI : MACHINGA RUKSA MWANZA
Rais magufuli aliyasema haya katika mkutano wa kufafanua shughuli za utendaji Serikali ya awamu ya Tano uliofanyika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza na kuhudhuriwa na ummati mkubwa wa wakazi wa mkoa wa Mwanza na wilaya zake.
"Sisi hatuna tatizo na Serikali yetu kabisa, kwasababu tuliichagua sisi wenyewe, tunatatizo kwamba kauli ya Mhe. Rais imefuatwa na kama ingefuatwa wala haya yasingekuwepo" Amesikika mmoja kati ya viongozi wa wamachinga.
Moja ya hoja zinazo weka utata, hata maeneo na viwanja walivyoelekezwa kwenda kufanya biashara kunautata kwamba baadhi ya maeneo hayo ni mali ya watu binafsi, nao wamekataa kata kata kuwaachia wafanyabiashara kufanya biashara.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment