ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 30, 2016

JAMII INAJITENGENEZEA BOMU LA BAADAE MALEZI YA SASA KILA MTU KIVYAKE MTOTO ANAJILEA MWENYEWE.

Balozi wa Ireland nchini Tanzania Paul Sherlock akihutubia mkutano wa wadau wa mtandao wa Kupinga vitendovya ukatili Kanda ya Ziwa uliofanyika jana Malaika Hotel jijini Mwanza. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.


Yasin Ally ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Kupinga vitendo vya ukatili ndani ya jamii (KIVULINI) amesema kuwa vitendo vya unyanyasaji vimekithiri na kuota mizizi nchini kiasi kwamba vinatishia hata usalama wa wadau hata wanaozungukwa na wasaidizi wa kisheria kutoka Serikalini.


MOJA YA MATUKIO MFANO.
MISUNGWI: Hii inaweza kuwa kali kuliko ulizowahi kuzisikia baada ya wanaharakati 13 waliokuwa kwenye mtandao wa kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi watoto wilayani hapa, Mkoa wa Mwanza kuenguliwa kwa kugeuka wanyanyasaji.
Taarifa kutoka ndani ya shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na kupinga vitendo hivyo la Kivulini, zilisema hatua hiyo imetokana na watu hao kubainika kujihusisha na vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya watu wengine, wakiwamo wake zao.
Uamuzi wa kuwaengua wanaharakati hao ambao ni miongoni mwa 100 wanaofanya kazi chini ya shirika hilo ulifikiwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kivulini, Yasin Ally baada ya kupokea taarifa ya tathmini ya kiutendaji kutoka kwa wenyeviti wa kata.

Kesi mbalimbali zinazohusu vitendo vya ukatili zimeripotiwa kwenye meza za jeshi la polisi.
Kusanyiko la wadau wa mtandao wa Kupinga vitendovya ukatili Kanda ya Ziwa uliofanyika jana Malaika Hotel jijini Mwanza. 
Wasemaji.
"Tumepokea taarifa za Vipigo, Kuchomwa moto, Matumizi ya silaha, Watu wamesukumwa ukutani na kuumizwa vibaya, kunyongwa baadhi ya sehemu zao za mwili, kuchomwa na vitu vyenye ncha kali, Kunyimwa haki za msingi na kadhalika"


Afande Mama Kotecha ambaye ni mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Ilemela naye alisimama kuto somo kwa moja ya vipengele ndani ya mkutano huo.

Jamii inatengeneza Bomu la baadae kwani malezi ya sasa kila mtu anaishi kivyake, mtoto amekosa malezi hivyo anajilea pekee. Nini Tofauti kati ya malezi ya wazazi wa zamani na wa sasa. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.

Kusanyiko la wadau wa mtandao wa Kupinga vitendovya ukatili Kanda ya Ziwa uliofanyika jana Malaika Hotel jijini Mwanza. 

Mwanaharakati Jimmy Luhende.
Picha ya hisia na majadiliano (Jimmy Luhende) akimwaga matirios mbele ya Mkutano wa wadau viongozi wa makundi ya mtandao wa Kupinga vitendovya ukatili Kanda ya Ziwa uliofanyika jana Malaika Hotel jijini Mwanza. 
Kusanyiko la wadau wa mtandao wa Kupinga vitendovya ukatili Kanda ya Ziwa uliofanyika jana Malaika Hotel jijini Mwanza. 
Balozi wa Ireland nchini Tanzania Paul Sherlock picha ya pamoja na wadau viongozi wa makundi ya mtandao wa Kupinga vitendovya ukatili Kanda ya Ziwa uliofanyika jana Malaika Hotel jijini Mwanza. 
Balozi wa Ireland nchini Tanzania Paul Sherlock picha ya pamoja na wadau viongozi wa makundi ya mtandao wa Kupinga vitendovya ukatili Kanda ya Ziwa uliofanyika jana Malaika Hotel jijini Mwanza. 
Picha ya wadau na viongozi wa makundi ya mtandao wa Kupinga vitendovya ukatili Kanda ya Ziwa uliofanyika jana Malaika Hotel jijini Mwanza. 
Mkutano ulimlizika nayo maadhimio yaliainishwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment