Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza mara baada ya kuwasili akitokea Chato mkoani Geita. |
Rais wa jamuhuli ya muungano wa Tanzania Dr.John Mgufuri amezitaka baraza za madiwani kufuta sheria ya kukusanya kodi kwa wakulima wadogo wadogo badala yake wakakusanye kodi kwenye maduka makubwa. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kutoa shukurani kwa wananchi Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza baada ya kutoka mapumziko mafupi wilayani Chato , amesema anaitaji kukusanya mapato sana lakini sio kwa wananchi wenye uwezo wa nchini ambao wanategemea kipato kutoka mashambani.
"Mkuu wa Mkoa na viongozi wenzako sikuwachangua ili mkae ofisi, nendeni kwa wananchi mkawaamasishe wananchi kufanya kazi za kilimo, uvuvi na ufungaji kwa kufanya hivyo tutaipekeka Tanzania yetu katika uchumi wa kati," kauli ya Magufuri.
"Wananchi fanyeni kazi kwa kujituma kw asabubu Selikali yangu haitokuwa tayari kutoa msaada wa Chakula katika wilaya ambayo itafanya uzembe wa kulima na kukusanya chakula kwa wakati, fedha ambazo ningenunua Chakula ni bora nizipeleke kwa watoto wa masikini ili waweze kusoma bure na kuboreshe miundombinu ya Elimu kama madarasa, walimu na vifaa vyakufundishia", aliongeza Magufuli
Nchi ilikuwa imefikia pabaya kwasababu ya watu wachache waliokuwa wanajinufaisha kwa kutumia fedha za wananchi masikini kitu ambacho siwezi kukifumbia macho nitawatumbua na ikiwezakana kuwakata miguu kabisa.
Rais Magufuli ameahidi kwa kipindi ambacho atakuwa madararakani amani ataisimama na hatokuwa tayari kuona amani ya nchi inayumbishwa na watu wachache, pia amewataka watanzania kudumisha amani na kutokubali kuyumbishwa na watu wachache ambao wanazingatia maslahi biafsi na si taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akizungungumza juu ya hali ya ulinzi na usalama, amesema mkoa umejizatiti kiusalama kuanzia ngazi zote chini hadi za juu kiasi kwamba hata matukio ya mauaji kwa vikongwe na watu wenye albinism yametoweka ikiwa ni mwezi wa nne sasa hayajatokea. |
Mamia ya wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza kwenye mkutano wa Rais Magufuli wilayani Sengerema mara baada ya kuwasili akitokea Chato mkoani Geita. |
Eneo la tukio viwanja vya Mnadani Sengerema. |
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dtk Charles Tizeba. |
Mamia ya wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza kwenye mkutano wa Rais Magufuli wilayani Sengerema mara baada ya kuwasili akitokea Chato mkoani Geita. |
Mbunge wa Jimbo la Sengerema William Ngeleja akifunguka juu ya miradi ya maendeleo inayoendelea jimboni humo kwake. |
Taswira. |
Kutoka Mwanza. |
Kutoka Mwanza. |
Mbunge wa Kwimba Shanif Mansoor. |
Mamia ya wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza kwenye mkutano wa Rais Magufuli wilayani Sengerema mara baada ya kuwasili akitokea Chato mkoani Geita. |
Mamia ya wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza kwenye mkutano wa Rais Magufuli wilayani Sengerema mara baada ya kuwasili akitokea Chato mkoani Geita. |
Aksanteni kwa kuja. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza mara baada ya kumaliza kuwahutubia. |
Selfie la Kibabe...Gsengo kutoka Jembe FM Mwanza. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.