Timu ya Simba Queens jana iliweza kuwaadhibu wapinzani wao Msimbazi Queens kwa 3-0 katika muendelezo wa mashindano ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars katika mkoa wa Ilala mchezo amba ulichezwa kwenye uwanja wa Karume.
Katika mchezo huo ambao ulianza huo ambao ulikuwa na kasi sana, timu ya Msimbazi Queens ndio walikuwa wa kwanza kufika langoni la wapinzani wao baada ya mshambuaji wake Rosemary Renatus kuwalamba chenga mabeki wawili wa Simba Queens na kuachia shuti dhaifu liliokolewa na kipa wa Simba Queens kwenye dakika ya 4 ya mchezo.
Msimbazi Queens waliendelea kusakama lango la wapinzani wao lakini hali ilibadilika kwenye dakika ya 17 baada ya Simba Queens kumtoa Zainabu Said na kumuingiza Eva Charles ambaye kwa kiasi kikubwa alibadilisha hali ya mchezo.
Hata hivyo, Simba Queens walibidi kusubiri mpaka dakika ya 36 kuandika mbao la kwanza. Ilikuwa Diani Hussein ambaye alichukua mpira katika ya uwanja na kutoa fursa murua kwa Zainabu Mohammed na kuandika mbao la kwanza.
Baada ya mbao hilo, Msimbazi Queens walionekana kuchanganyikiwa kitu ambacho kilitoa nafasi kwa Simba Queens kuandika mbao. Mbao hilo lilitokana na beki wa Msimbazi Fatuma Shabaan kushindwa kucheza mpira uliorudishwa kwake na beki mwenzake Salma Masoud na kusababisha mshambualiaji wa Simba Queens Zainabu Mrisho kuifungia timu yake mbao la pili kwenye dakika ya 38 ya mchezo.
Simba Queens waliendelea kutawala mchezo na mnamo dakika ya 48, mchezaji ambaye aling’ara katika mchezo huo Zainabu Mohammed alishirikiana vema na mshambuaji mwenzake Eva Charles na kutoa pasi kwa Sarah Ramadhan aliweza kuifungia timu yake goli ya tatu.
Katika mchezo mwingine uliochezwa katika uwanja huo Ilala Queens waliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Ukonga Queens, bao ambalo lilipatikana katika dakika ya 17 ya mchezo mfungaji akiwa ni Jane Claus.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.