MBUNGE wa jimbo la mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa akihutubia wananchi waliofika kwenye mkutano uliyafanyika kwenye shule ya sekondary Mdabulo. |
Baadhi ya wananchi waliokuwa wamehudhuria mkutano huu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini mahamood mgimwa. |
MBUNGE wa jimbo la mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa akikabidhi mifuko 100 ya saruji na ndoo kumi za rangi zenye ujazo wa lita ishirini kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya ya kukarabati majengo ya shule ya sekondari ya Mdabulo kwa uongozi wa wilaya ya mufindi. |
Na fredy mgunda,mufindi
MBUNGE wa jimbo la mufindi
kaskazini Mahamood Mgimwa amekabidhi mifuko 100 ya saruji na ndoo kumi za rangi
zenye ujazo wa lita ishirini kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya ya
kukarabati majengo ya shule ya sekondari ya Mdabulo iliyopo Kijiji cha Mdabulo
wilayani mufindi.
Akihutubia mkutano wa
hadhara uliofanyika kijijini Mdabulo, alisema kuweza kujenga jamii imara ni
lazima kuhakikisha elimu inapewa kipaumbele cha pekee.
“Sina budi kuunga mkono
juhudi zenu za ujenzi wa Shule ya sekondari ya Mdabulo, ambayo imejengwa kwa
nguvu za wananchi, nami kama mwakilishi wetu ninaungana nanyi kwa dhati na
katika hili napenda kukabidhi mifuko ya saruji.
huo.
Alisema lengo la kutoa
msaada huo, ni kutokana na shule hiyo kuwa chakavu katika maeneo muhimu kama kwenye
mabweni na bwalo ambalo hutumiwa na wanafunzi kwa ajili ya chakula.
“Baada ya kupata taarifa
hizi, nimeamua kuja na mkuu wa wilaya pamoja na mkurugenzi ili waangalie namna
ya kufanya marekebisho katika madarasa pamoja na mabweni ya shule hii na nimewaagiza
wahakikishe wanakarabati shule hiyo na iwe kwenye viwango vinavyotakiwa,”
alisema Mgimwa.
Mgimwa aliwataka wanafunzi
wasome kwa bidii ili waweze kufaulu na si kusoma ili kupata ajira kama
ilivyozoeleka kwa watu wengi kwani serikali inafahamu changamoto ya ajira
iliyopo.
Hata hivyo aliwataka wazazi
na walezi kuwalea watoto katika maadili mema huku wakisaidiana na walimu kwa
kushirikiana katika nyanja ya elimu ili kupanua wingo wa ufaulu kwa wanafunzi.
“Kwa kipindi cha siku kadhaa
nimekuwa na ziara katika katika jimbo langu kwa lengo la kutimiza ahadi zangu
pamoja na kusikiliza kero ya wananchi na kero moja wapo ni wazazi
kutowajali wanafunzi wala kutojua
maendeleo ya watoto wao pindi watokapo shule”alisema Mgimwa.
Naye Mwalimu Mkuu wa shule
hiyo, Geogrge Mgomba, aliwataka wanafunzi wake kusome kwa ajili ya ajira
binafsi na si kutegemea ajira kutoka serikalini kwa kuwa serikali ina mzigo
mkubwa.
“Wanafunzi mnatakiwa msome
kwa bidii na msitegemee ajira kutoka serikalini, mtafute ajira binafsi au
kujiajiri wenyewe,”alisema
Kwa upande wake,mkuu wa
wilaya ya mufindi Jamhuri Wiliamu, alimshukuru mbunge huyo kwa kuunga mkono
juhudi za wananchi za kuinua sekta ya elimu katika wilaya hiyo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.