Mkazi wa Kitongoji cha Bomani, Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Suzana Dizama (58) amefariki dunia baada ya kuungua na moto wa kibatari ulioshika chandarua wakati akiwa amelala.
Akizungumzia tukio hilo, kaka wa Suzana, Dabirian Kinyolo alisema jana kuwa mdogo wake alirudi nyumbani usiku akitokea kilabuni kunywa pombe, alifika na kuwasha kibatari karibu na kitanda chake jambo lililosababisha moto kushika chandarua.
Kinyolo alisema katika tukio hilo wajukuu wawili wa Suzana ambao ni Ratifa Siyajali (4) na Rehema Siyajali (2), walinusurika baada ya kukimbia kutoka ndani walipoona moto unazidi.
“Kwa sababu Suzana alikuwa amelewa sana, alishindwa kukimbia hivyo kuteketea akiwa ndani ya nyumba,” alisema Kinyolo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.