Press Release
Airtel Money yagawa billion 3 kwa wateja na Mawakala
Dar es Salaam, Jumanne 23 Agosti 2016, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetoa gawio la faida la kila kiasi cha shilingi billion 3 kwa wateja wake wa Airtel Money na mawakala wakubwa na wadogo nchi nzima
Airtel imetoa gawio la faida kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi juni mwaka huu ambapo kila mteja atalipwa sehemu ya faida kulingana na kiasi cha salio lake katika akaunti yake ya Airtel Money kila siku
Akiongea na waandishi wa habari , Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando alisema “Tunayofuraha kutoa gawio la faida la shilingi bilioni 3 kwa wateja wetu na wakala nchi nzima. Tunaamini gawio hili la faida litawawezesha wateja wetu kutatua mahitaji yao ya kifedha na hivyo kuthibitisha dhamira yetu ya kuendelea kutoa huduma za kifedha”
“Tumejipanga kuwawezesha wateja wetu kwa kupitia huduma na bidhaa tunazozitoa. huduma ya Airtel Money imelenga kuleta unafuu na kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha katika maeneo mbalimbali nchini hususani ya maeneo ya pembezo mwa nchi. Aliongeza Mmbando
Mpaka sasa Airtel imeshatoa kiasi cha shilingi billion 10 kwa wateja na mawakala wa Airtel money tangu 2014
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.