ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 16, 2016

YANGA YAAMBULIA POINTI MOJA MZUNGUKO WA KWANZA KOMBE A SHIRIKISHO AFRIKA.

Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
YANGA SC imekamilisha mechi za mzunguko wa kwanza wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika bila ushindi, kufuatia kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Medeama ya Ghana jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga iokote pointi ya kwanza, baada ya awali kufungwa 1-0 mara mbili mfululizo na MO Bejaia nchini Algeria na TP Mazembe ya DRC Dar es Salaam pia.

Yanga inaendelea kukamata mkia kwenye kundi lake, wakati Medeama inabaki nafasi ya tatu kwa pointi zake mbili, nyuma ya MO Bejaia yenye pointi nne na TP Mazembe pointi sita. 

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Ibrahim Nour El Din, aliyesaidiwa na washika vibendera Ayman Degaish na Samir Gamal Saad wote wa Misri, hadi mapumziko tayari timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.