Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na badhi ya wananchi wa Kijiji cha Ipala. Dk. Kigwangalla amewataka wananchi hao kuendelea kusubiria kwani tatizo hilo analitatua kwa njia ya mazungumzo na tayari Waziri mwenye dhamana amekubali kufika eneo hilo kwa ajili ya kujionea. (Picha zote na Andrew Chale,Nzega-Tabora). |
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla amewaomba wananchi wa Kijiji cha Ipala ambao wamekuwa na mgogoro wa muda mrefu na watu hifadhi ya Msitu wa Ipala kuwa na subira kwa kipindi hiki kwani tatizo lao linashughulikiwa ambapo Waziri mwenye dhamana anatarajiwa kufika kwenye kijiji hicho kwa ajili ya hatua Zaidi za kitatuzi.
Kijiji hicho cha Ipala chenye Zaidi ya Kaya 700, Wanakijiji wake wamekuwa wakiishi huko kuanzia mwaka 1952 ambapo wameendelea kuishi humo na familia na kufanya shughuli zao za kijamii za kila siku Dk. Kigwangalla amesema kuwa, tayari Serikali suala hilo wanalitambua hivyo wanatumia njia za mazungumzo katika kutatua mgogoro huo kwa sasa wanatarajia ujio wa Waziri Mwenye dhamana kutembelea eneo hilo.
“Matatizo yenu nayajua na Serikali pia inalifahamu suala hili muda mrefu hivyo nawaomba wananchi muwe na subira kwa kipindi hiki na mimi Mbunge wenu natarajia kurudi hapa na Mh. Waziri wa Maliasili na Utalii na atafika huku kuja kushuhudia mgogoro huu.” Alieleza Dk. Kigwangalla kwa wananchi hao huku akishangiliwa na wanakijiji hao waliofurika kwa wingi katika eneo la uwanja wa kituo cha Ipala.
Tazama MO tv, Dk. Kigwangalla alipohutubia Wanakijiji hao wa Ipala hapa:
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwasili kwenye kijiji cha Ipala huku akipokelewa na baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo
Msululu wa wananchi wakiwa wamempokea Dk. Kigwangalla wakati akiwasili kwenye kijiji cha Ipala.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.