ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 13, 2016

ALIYEWAUA WATU FLORIDA ALIKIRI KUUNGA IS MKONO

Mateen.
Shirika la ujasusi la Marekani- FBI, limesema mtu aliyewaua watu 50 kwa kuwafyatulia risasi katika klabu moja ya wapenzi ya jinsia moja huko Florida, alikiri kuunga mkono kundi la kigaidi la IS, lakini hawakumuona kama mtu hatari.
Mateen, anasemekana kupigia simu mamlaka ya kitaifa ya maswala ya dharura muda mfupi kabla ya kuanza kuwapiga watu risasi huku akisema kuwa anaunga mkono kundi la IS.
FBI wameongeza kusema kuwa wamekuwa wakimfanyia uchunguzi mtu huyo tangu 2013 baada ya kutoa matamshi ya chuki akiwa kazini.
Wakati alipotoa matamshi hayo ya chuki, alikuwa na uhusiano na mhanga mmoja aliyejilipua nchini Syria.
Mateen aliendelea kufanya kazi kama mlinzi wa usalama huku akinunua silaha kisheria.
Seddique Mir Mateen speaks to reporters about his son, Omar Mateen, the 29-year-old Orlando shooter. (AP Photo/APTN)
Seddique Mir Mateen akizungumza na waandishi wa habari juu ya maisha ya kijana wake aliye tekeleza mauaji hayo, Omar Mateen.
Babake Mateen amesema anaamini kitendo alichokifanya mwanawe kilitokana na msukumo wa hisia zake dhidi ya wanaondeleza mapenzi ya jinsia moja na wala si kwa sababu za kidini.
Maombolezo juu ya tukio hilo la simanzi kubwa. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.