ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 13, 2016

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AAPISHWA NA KUPOKELEWA MAKAO MAKUU YA WIZARA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh, Mwigulu Nchemba(kushoto), muda mfupi baada ya Sherehe ya Kumwapisha iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh, Mwigulu Nchemba(kulia), na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni, muda mfupi baada ya Rais Dkt. John Magufuli kumwapisha Waziri Mwigulu Nchemba kuongoza wizara hiyo leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mwigulu Nchemba(Kushoto), akikaribishwa Makao Makao ya Wizara hiyo na Katibu Mkuu Meja Jenerali Projest Rwegasira.Katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Hamad Masauni na wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Balozi Yahya Simba.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Mawasiliano, Jane Massawe, mara baada ya kupokelewa Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akiweka saini mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi muda mfupi baada ya kuapishwa kwake. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Yahya Simba.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi). 
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha mawaziri wapya wa mambo ya ndani na yule wa kilimo siku mbili tu baada ya kutangaza mabadiliko madogo katika baraza lake la mawaziri.
Jumamosi iliyopita rais Magufuli alitangaza uteuzi wa mbunge wa Buchosha Dkt. Charles John Tizeba kuwa waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi.
Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, bwana Mwigulu Lameck Nchemba aliteuliwa kuwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchi.
Bwana Nchemba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani bw Charles Muhangwa Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Mawaziri hao walikula kiapo cha uaminifu kwa rais na jamhuri ya tanzania saa tatu asubuhi katika ikulu ya rais jijini Dar es salaam.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.