07:45 Upigaji kura katika maeneo mengi umeanza, ingawa kwa kuchelewa. Hapa ni Kalangala watu wakipiga kura.
07:44 Kuna ripoti kwamba baadhi ya watu wanaotumia simu kuingia mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook wanatatizika. Lakini WhatsApp inafanya kazi.
07:30 Upigaji kura ulifaa kuanza saa moja asubuhi lakini katika vituo vingi, licha ya wapiga kura kujitokeza, shughuli yenyewe haijaanza na wapiga kura wanalalamika. Katika kituo cha Kamwokya Central Market, vifaa vya kupigia kura vinaingizwa kituoni pole pole. Mwangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya Madola Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo amekuwa katika kituo hicho.
07:09 Tuangalie takwimu muhimu kuhusu uchaguzi wa Uganda unaofanyika leo.
Takwimu muhimu | |
---|---|
Wagombea urais | 8 |
Maeneo bunge | 290 |
Vituo vya kupigia kura | 28,010 |
Wapiga kura waliosajiliwa | 15,277,196 |
06:40 Wapiga kura wameanza kufika katika vituo vya kupigia kura. Hapa ni katika kituo cha Kalangala, katika kisiwa kilichoko katika Ziwa Victoria.
ZAIDI:- BBC SWAHILI
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.