Wanahabari na Watafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), waliokuwa katika ziara ya kuzungumza na wakulima wa mkoa wa Mwanza kuhusu changamoto za kulimo zinazo wakabili pamoja na matumizi ya bioteknolojia katika kilimo wakiwa mbele ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere walipozuru kaburi hilo hivi karibuni Kijiji cha Mwitongo Butiama mkoani Mara.
Watafiti na wanahabari hao wakiwa mbele ya makaburi ya wazazi wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
Mtafiti Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknnolojia (Costech), Dk.Nicholaus Nyange (kushoto), na Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Emmarold Mneney wakiwa wamesimama ilipo sanamu ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Hapa ni picha ya pamoja katika sanamu ya Baba wa Taifa.
Mwendeshaji wa mtandao wa www. habari za jamii.com Dotto Mwaibale akivinjari katika moja ya jengo katika makazi ya Baba wa Taifa.
Matembezi yakiendelea katika makazi ya Baba wa Taifa.
Mratibu Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Afrika, Daniel Otunge (kushoto) Mtafiti Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknnolojia (Costech), Dk.Nicholaus Nyange (katikati), na Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Emmarold Mneney wakiwa wamekaa katika kibanda alichokuwa akipenda kupumzika Hayati Nyerere wakati wa
uhai wake.
Jamii inayofanya shughuli mbalimbali nyumbani kwa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere wakionesha upendo kwa kunywa chai pamoja katika makazi ya Mwalimu Nyerere yaliyopo Kijiji cha Mwitongo, wilayani Butiama mkoani Mara kama walivyonaswa na kamera yetu katika ziara hiyo.
Picha ya pamoja katika nyumba maalumu lilipo kaburi na Mwalimu Nyerere.
Dereva wa Msafara huo, Mr Stanley akiwa mbele ya gari na mtafiti Kutoka Kituo cha Utafiti cha Ukiriguru cha jijini Mwanza, Isabela Msuya.
Mwendeshaji wa mtandao wa www. habari za jamii.com Dotto Mwaibale akiweka maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.