Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa BAWACHA na Mbunge Viti
Maalumu Taifa Grace Tendega (katikati) jana February 20,2016 akizindua
ofisi Mpya ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Chadema, Susan
Masele (Kulia). Kushoto ni Paschazia Renatus ambae ni Katibu wa Bawacha
Mkoa wa Mwanza.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Chadema, Susan Masele akizungumza katika uzinduzi wa ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema). |
"...Kazi ya Mbunge siyo kugawa hela. Kazi ya Mbunge ni kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua. Na mimi niseme nitakuwa mwakilishi bora na hapa tumeanza tu ambapo katika ofisi hii nitakuwa napokea na kusikiliza kero za wananchi na kwenda kuzisemea bungeni... Alisema Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Chadema, Susan Masele.
Ofisi hiyo inapatikana Mtaa wa Ghana Green View, Kata ya Nyamanoro, Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza. Ndani yake pia kuna Ofisi ya BAWACHA Mkoa wa Mwanza.
Taswira kwa ndani. |
Ofisi kwa ndani. |
Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa BAWACHA na Mbunge Viti Maalumu Taifa Grace Tendega akiweka saini katika kitabu cha wageni ofisini hapo. |
Engo ya wanahabari waliojitokeza tukioni. |
Akina mama wa Chadema wakiwa katika uzinduzi wa ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema).
Bendera za Taifa na Chadema zikipandishwa wakati wa uzinduzi wa ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema).
Kabla ya Uzinduzi huo, Kulikuwa na Shughuli ya Kuwatembela wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure ikiwa ni pamoja na kutoa zawadi kwa akinamama kama pongezi ya uvumilivu.
Kaimu mganga mkuu hospitali hiyo akitoa ufafanuzi wa changamoto zilizopo hospitali ya Sekou Toure.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.