Mwenyekiti wa CCM Taifa Dr Jakaya Mrisho Kikwete wakati akizindua Jengo la CCM Kibaha mji katika hafla iliyofanyika katika ofisi hiyo. |
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka kulia akimpa historia fupi kuhusina na ujenzi wa jingo hilo Mwenyekiti wa CCM Jakaya Kikwete kulia kabla ya kufanyika kwa uzinduzi huo. |
Mwenyekiti wa CCM Jakaya Kikwete kushoto akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na CCM wakati alipowasili katika ofisi hizo kabla ya kufanyika kwa uzinduzi, (Picha zote na Victor Masangu) |
PM NA VICTOR MASANGU, PWANI
MWENYEKITI wa CCM na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne, Dr.Jakaya Kikwete ameagiza viongozi wa Chama kuanza kuwekeza kwenye rasilimali za chama ili kujenga uwezo wa chama na kuachana na tabia ya kuwa tegemezi.
Jakaya alisema kwamba kuna Chama kina udhaifu katika eneo hilo hivyo aliagiza wilaya zote zianze kuweka utaratibu wa kukiwezesha chama kuwa na uwezo wa rasimali fedha. Aliagiza viongozi wa CCM kuanzisha mifuko ya uchaguzi mkuu ujao kwa kuwa maandalizi yanapaswa kuanza sasa kuwa miaka mitano sio mingi.
Kikwete alisema chama kinatakiwa kuwa rasilimali fedha, ofisi zenye hadhi,vyombo vya usafiri ili kiweze kuwafikia wanachama na kujiimarisha. Alisema jeshini kuna msemo unaotumika usemao kwamba jasho jingi wakati wa amani ,damu kidogo wakati wa vita.
Mwenyekiti alisema maandalizi yakifanyika mapema kwa kuweka kidogo kidogo wakati wa uchaguzi hakutakuwa na kazi kubwa. Alisema baada ya Rais Dk.John Magufuli baada ya kuapishwa rasmi...maandalizi ya uchaguzi ujao wa 2020 yanatakiwa kuanzia hapo.
Akizungumzia kuhusu waliokihujumu chama.Mwenyekiti huyo wa CCM alisema lazima wadhibitiwe kwa kuwa kuhujumu ni kosa. "Aliyetuhujumu na kutomuunga mkono mgombea wa CCM sio mwenzetu.Tuliagiza vikao vikae watu waitwe waambiwe ukweli, Alisema na kuongeza kuwa vikao vifanye uamuzi kwa kutenda haki...bila kumuonea na viongozi wasififishe demokrasia.
Katika hatua nyingine Kikwete lipongeza Mbunge wa Kibaha Mjini Silvestry Koka kwa uamuzi wake wa kuamua kujitolea fedha kwa ajili ya ujenzi huo na kuwataka viongozi wengine kuiga mfano huo wa kujitolea katika kukisaidia chama.
“Mheshimiwa koka amefanya jambo kubwa sana kwani ameweza kujitolea kwa moyo mmoja katika kutoa faedha yake yeye katika kukisaidia chama huu ni mfano wa kuiga kwa viongozi wengine kuiga mfano huo wa Koka ni jambo kumbwa la kumpongeza kwa hatua ambayo ameifanya,”alisema Kikwete.
Kadhalika aliwataka wana CCM wamuunge mkono Dk.Magufuli kwa kuwa anayotekeleza ni maelekezo ya ilani ya uchaguzi ya CCM. "Masuala ya kudhibiti rushwa,wazembe kwenye kazi na kuimarisha makusanyo ya kodi ili kujenga uchumi yamo kwenye ilani, hivyo wana CCM tukimuunga mkono tunampa nguvu yeye na serikali take"alisema Alisema viongozi wa serikali ya awamu ya tano wako mstari wa mbele kwenye mapambano na wana CCM wanapaswa kufuata nyuma kwa kuunga mkono mapambano.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM..Kibaha Mjini,Maulid Bundala alimuomba Mwenyekiti huyo..kushughulikia suala la wananachama ambao wamehusika kukiuhujumchama na kusababisha kupunguza kura za CCM.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvesrty Koka aliesme kwamba ameamua kufanya uamuzi wa kujenga ofisi hiyo ya chama kwa ajili ya viongozi wake waweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
“Mimi na familia yangu nimeamua kutoa kisi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya chama kwani hapo awali ofisi ilikuwa eneola maili moja sehemu ambayo iikuwa ni ndogo hivyo kukamilika kwa ujenzi huu pia utaweza kurahisisha ufanyaji kazi na kuweza kukijenga chama chetu,alisema Koka.
Alisema wapo wanachama ambao wanaingia CCM kama njia ya kusaka vyeo lakini hawana uchungu na chama ..wakikosa wanahujumu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.