ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 12, 2015

WAKATI MAREKANI WAKIADHIMISHA SIKU YA PANYA DUNIANI, TANZANIA BADO MNYAMA HUYO NI ADUI SIKILIZA WATAALAMU NA WANANCHI WANASEMAJE.

Watangazaji wa kipindi cha **HIT ZONE** ya Jembe FM Mwanza kinachoruka mchana saa saba hadi kumi kamili (13:00 - 16:00) kutoka kushoto ni @mbabavc @nattyebrandy na mkali toka Jembe DJz @chrissthedj ambapo leo wamehusika kutoa mpango mzima wa taarifa ya siku ya SIKU YA PANYA DUNIANI.
Kila Inapofika NOVEMBER 12 (Siku kama Ya Leo), Nchini marekani , na baadhi ya nchi ulimwenguni, ni Maadhimisho ya Siku ya Panya Duniani (Fancy Rat & Mouse Day).

Siku hii huwa ni maalum Kwa ajili ya kutambua haki na Thamani ya Mnyama huyu, ambaye kwa asilimia kubwa, kwa baadhi ya mataifa ikiwemo baadhi ya mikoa hapa nchini Tanzania imekuwa ikimchukulia kama Mharibifu wa Vitu mbali mbali, mazao, mali, matandiko nakadhalika.

Taasisi iliyopewa Jina la AFRMA (American Fancy Rat & Mouse Association), Ndiyo inasimamia Shughuli zote hasa katika Kuhakikisha Panya Wanapewa haki zao za Msingi kama Ilivyo kwa wanyama wengine.
Kwa wengine ni chakula.

KWANINI SIKU YA PANYA INAADHIMISHWA
Siku ya Panya Huadhimishwa Kwa sababu Mbali mbali , ingawa Kwa Uchache ni kama Ifuatavyo:
1.            PANYA huchukuliwa/hutafsiriwa Kama Mnyama au kiumbe ambacho ni hatari kwa maisha ya Binadamu, ikiwemo kuambukiza magonjwa kadhaa
2.            PANYA hutafsiriwa kama Kiumbe ama Mnyama Mharibifu .
3.            PANYA hastahili kupata Haki za Mnyama, hasa ukizingatiani Adui Mkubwa wa Binadamu, akihusishwa na makundi Mengine ya Wanyama na wadudu ambao ni adui kwa Binadamu

Wadau wa kipindi cha HIT ZONE ya Jembe FM Mwanza kutoka kushoto ni @mbabavc @nattyebrandy na mkali toka Jembe DJz @chrissthedj 
NAMNA AMBAVYO SIKU YA PANYA INAADHIMISHWA:
AFRMA, iliyoanzishwa Mwaka 1983, califonia, Nchini marekani, mara kwa mara Hufanya yafuatayo katika  Maadhimisho ya Siku ya Panya
1.            Michezo Mbali mbali ama mashindano mbali mbali ambayo huwahusisha panya Wa Kufugwa (Domestic rats & Mouse)
2.            Kutengenezwa vitu mbali mbali vyenye muonekano wa Panya
3.            Kuwakutanisha Panya Wanaofugwa na watu tofauti na katika mazingira Tofauti
4.            Kutatua matatizo mbali mbali ambayo yanawaandama Panya
5.            Monesho mbali mbali kuhusu panya , mfano, Fashion, Chakula cha panya, dawa za panya, muonekano wa Panya, Vitu vya kuwahifadhi panya, na mengineyo. ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA
NCHINI TANZANIA: PANYA BADO ANABAKI KUWA ADUI NA MNYAMA MHARIBIFU.
Kwa Mujibu wa Mtaalamu wa kilimo na Mifugo Jijini Mwanza, Bw. Aboubakar Burhani, ambaye pia ni Mfanya Biashara wa Sumu za Panya, Mnyama Huyu bado anatafsiriwa kama Kiumbe Mharibifu, na adui kwa wananchi mbali mbali.

Bw. Burhani ameongeza kuwa, Panya amekuwa akichukiwa na Wananchi, sababu huharibu vitu mbali mbali vya Binadamu, mfano Nguo, mazao, na thamani.

Pia ameongeza Kuwa, Kwa nchi ya Tanzania na nchi Nyinginezo za Afrika, hazijafikia hadhi ama maamuzi ya Kumpa panya hadhi na haki ya Kusherekea Siku yake, labda kama itatokea Miaka ya Mbele kabisa.

Kwa Upande wao baadhi ya wananchi Jijini Mwanza, wamezungumza kwa Nyakati tofauti kuhusu Mnyama PANYA, huku wakidai kuwa Mnyama Huyu ni Mharibifu, nab ado atabaki katika Tafsiri Hiyo hiyo.


Wengine wameshauri kuwa, Panya ambao ni wa porini, waandaliwe siku yao Maalum, maana sio waharibifu kama wengine, na kwa asilimia kubwa hutumika kama Kitoweo kwa Baadhi ya jamii, hutumika katika shughuli za utafiti, pamoja na uteguaji mabomu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.