Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, Justus Kamugisha |
Novemba 4,2015.
SHINYANGA.
Wananchi mkoani Shinyanga wametakiwa kuwa watulivu kwa kutokukubali vishawishi vya watu wanaotaka kuvunja amani katika kipindi hiki Taifa likisubiri kuapishwa kwa Rais mteule Dk.John Pombe Magufuli.
Kauli hiyo imetolewa leo na kamanda wa Polisi mkoani humo wakati akizungumza na Jembe Fm na kusema kuwa wananchi wanatakiwa kuwa makini na kuepuka kurubuniwa na watu ili kuvunja amani iliyopo nchini.
Kamugisha amesema kuwa wananchi hawana budi kuitunza amani iliyopo hivi sasa na ikipotea ni vigumu kuirejesha baada ya kutoweka kama mataifa mengine yaliyoingia kwenye machafuko wananchi wake wanajutia kupotea kwake.
Ameongeza kuwa LEO ni siku ya kuapishwa kwa Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli hivyo ni vyema wananchi wakaitumia siku hii kwa uangalifu kwa kuwa vyombo vya usalama mkoani humo havitakuwa nyuma kumshughulikia yeyote atakebainika kuvunja amani.
Hata hivyo Kamugisha amewashukuru wananchi kwa watulivu na utii waliouonesha jana ambapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,kilipanga kufanya maandamano ambayo yalipingwa na Jeshi la Polisi.
Wakati huo huo jijini Mwanza Polisi wameonekana kutanda maeneo mbalimbali wakiwa na mavazi rasmi wakizunguka huku na kule kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.