KATIBU msaidizi CCM wilaya ya Nyamagana mkoa wa Mwanza Mustapha Hanigwa ameweka bayana masuala mbalimbali yaliyojitokeza na hata kutokea ucheleweshwaji wa matokeo ya uchaguzi nafasi ya ubunge wilaya hiyo kongwe iliyo katikati ya mji wa Mwanza ambayo ndiyo yenye kubeba hadhi ya jiji.
Amesema kuwa sheria za Uchaguzi zinaruhusu mgombea kuingia kwenye chumba cha kuhakiki mahesabu ya kura akiwa na wakala wake.
Wengine wanaoruhusiwa ni Askari polisi, Mkurugenzi ambaye ni msimamizi wa uchaguzi na wasaidizi wake, Maafisa wa tume ya taifa ya uchaguzi (akina Jaji Lubuva, Mkurugenzi na watu wengine toka Tume)
Wadau wengine wanaoruhusiwa kuingia ni Waangalizi wa Kimataifa ambapo kulikuwa nawadau toka Finland, Marekani, Canada na Mataifa mengine nia ni kuhakikisha kuwa haki inatendeka.
Mwingine yeyote haruhusiwi kuingia kwenye chumba husika awe Mkuu wa Mkoa, Katibu wa Chama au awaye yeyote ambaye hajaainishwa hapo juu hata Rais wa nchi haruhusiwi.
Wagombea wengine wote walitimiza masharti isipokuwa mgombea wa CHADEMA Ezekiel Wenje ambaye licha ya kuwa na wakala wake alikuwa akilazimisha watu wake wengine 7 kuingia kwenye chumba cha kuhakiki. Hapo ndipo utata ulipozuka.
BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Wananchi pamoja na wanachama waliojitokeza katika mkutano wa shukurani uliofanyika kwenye viwanya vya Shule ya Msingi Mbugani jijini Mwanza. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.