ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 12, 2015

AMINI USIAMINI SASA WATEJA WA AIRTEL KUTUMA PESA BURE!!

Meneja Uhusiano wa Airtel , Jackson Mmbando akionge na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ofa kwa wateja wake itakayowawezesha kutuma pesa kiasi chochote cha pesa kupitia huduma ya Airtel Money bure. Pichani ni Stephen Kimea Meneja kitengo cha Airtel Money ( kushoto) na Aliesikia Peter Afisa kitengo cha Airtel Money.
Meneja Uhusiano wa Airtel , Jackson Mmbando (katikati) pamoja na Meneja kitengo cha Airtel Money, Stephen Kimea ( kushoto) na Afisa kitengo cha Airtel Money, Aliesikia Peter kwa pamoja wakionyesha kipeperushi cha ofa mpya itakayowawezesha wateja wa Airtel kutuma pesa kiasi chochote cha pesa kupitia huduma ya Airtel Money bure.

WATEJA wa Airtel kutuma pesa bure * Kutuma pesa Airtel kwenda Airtel bila kikomo Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua ofa kabambe itakayowawezesha wateja wa Airtel Money kutuma pesa kwa marafiki na familia zao ndani ya mtandao wa Airtel Bure Ofa hii mpya ijulikanayo kama "Okoa Mapene'' ina lengo la kuinua huduma za kifedha na kuwapatia wateja njia rahisi ya kufanya miamala yao ya kila siku 

Akiongea wakati wa uzinduzi, Meneja Uhusiano wa Airtel Bwn Jackson Mmbando alisema " kwa mara nyingine tena tunadhirisha kwa vitendo dhamira yetu ya kutoa huduma za kibunifu, rahisi na zenye gharama nafuu kupitia huduma ya Airtel Money.

Leo tunawawezesha wateja wetu wa Airtel money nchi nzima kuokoa pesa wanapotuma pesa kwenda kwa mtumiaji wa Airtel kwani tozo za kutuma pesa ni BURE kwa kiasi chochote kitakachotumwa.

Tunaamini ofa hii ya "Okoa Mapene'' itakuwa kichocheo kikubwa kwa wateja kutumia huduma ya Airtel Money kwa muda wa mienzi mitatu na zaidi" Aliongea kwa kusema "Okoa Mapene'' ni njia mojawapo ya kuwazawadia wateja wetu wanaotuma pesa kwa ndugu , jamaa, marafiki, familia na washirika wao wa biashara kupitia huduma ya Airtel Money. 

 "Okoa Mapene'' pia kuwawezesha mawakala kupata kamisheni zaidi kutokana na kuwa na wateja wengi watakaofanya miamala mingi kuanzia sasa. Ili kupata kutuma pesa mteja anatakiwa kupiga *150*60# na kuunganishwa kwenye menu ya Airtel Money na kuanza kufanya miamala yake BURE.

Hivi karibuni Airtel imewazawadia wateja wake kwa kuwapatia gawiwo la faida watumiaji wote wa huduma ya Airtel Money na kuwawekea gawiwo hilo moja kwa moja kwenye akaunti zao za simu. Mwisho

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.