ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 12, 2015

ACT-WAZALENDO WATAKA KUMALIZWA KWA MKWAMO WA KISIASA ZANZIBAR.

CHAMA cha ACT WAZALENDO kimemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kuisimamia tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC kutangaza matokeo ya kiti cha urais ama kurudia uchaguzi mzima, ikishindikana, rais atangaze hali ya hatari visiwani humo.

Kiongozi Mkuu wa Chama hicho Zuberi Kabwe amesema hali ya sasa Zanzibar siyo nzuri hivyo ni vyema Rais kulipa uzito wa kipekee na kulishughulikia kwa haraka suala hilo ili kuiweka nchi katika hali ya amani ambayo imekuwa sifa kwa taifa letu kipindi kirefu.

Hata hivyo Kabwe amesifu kasi ya utendeji kazi ya Magufuli akisema kuwa inatia matumaini ya kuipeleka Tanzania kwenye maendeleo ya kweli na kushauri juhudi hizi zikaelekezwa pia Zanzibar ili kuleta hali ya utulivu visiwani humo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.